Makamu wa Rais, Samia Hassan Saluhu, akimkabidhi tuzo maalum Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela wakati wa Wiki ya Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, ambapo benki hiyo ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo. (Picha na Francis Dande).
Makamu wa Rais, Samia Hassan Saluhu, akimkabidhi cheti cha shukrani Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, kwa udhamini mkuu wa Wiki ya Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani.Ofisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Ninael Munuo, akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu kuhusu huduma zitolewazo na benki hiyo ikiwemo simu akaunti.
Ofisa Masoko Mwandamizi wa Benki ya CRDB, Ninael Munuo, akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu kuhusu huduma zitolewazo na benki hiyo ikiwemo SimAccount.
Makamu wa Rais akimpongeza Mkurugenzi wa Benki ya CRDB.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa, wakimpongeza Ofisa Masoko Mwandamizi wa benki hiyo, Ninael Munuo, baada ya kuvutiwa na maelezo aliyoyatoa kwa Makamu wa Rais, Samia Hassan Suluhu, kuhusu huduma zitolewazo na benki hiyo ikiwemo SimAccount, wakati wa Wiki ya Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani.
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja wa Benki ya CRDB, Tully Mwambapa, akitoa maelezo mafupi kwa Makamu wa Rais Samia Hassan Suluhu namna Benki ya CRDB ilivyodhamini wajasiriamali wa Mkoa wa Kibaha katika Wiki ya Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani. Kulia ni Katibu wa Jukwaa Uwezeshaji Wanawake Kiuchumi Mkoa wa Pwani, Edna Mgonja.
Makamu wa Rais, Samia Hassan Saluhu, akimpongeza Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela baada ya kutoa hotuba yake wakati wa Wiki ya Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, ambapo benki hiyo ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
Makamu wa Rais, Samia Hassan Saluhu, akipongezwa na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela baada ya kutoa hotuba yake wakati wa Wiki ya Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani, ambapo benki hiyo ni mdhamini mkuu wa maonyesho hayo.
Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB.
Maofisa wa benki wakiwa na tabasamu tayari kuwahudumia wateja
Maofisa wa Benki ya CRDB wakimsikiliza mgeni rasmi alipotembelea banda la Benki ya CRDB.
Maofisa wa Benki ya CRDB wakiwa katika maandalizi ya kutoa huduma katika banda lao.
Kibaha, Tanzania
MAKAMU wa Rais, Mama Samia Hassan Suluhu ameipongeza Benki ya CRDB kwa kudhamini Wiki ya Maonyesho ya Viwanda Mkoa wa Pwani kwa kuwa yanatoa fursa na hamasa ya juu kwa uwekezaji kwenye viwanda na kufungua masoko ya bidhaa za viwanda hivyo.
Akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi rasmi wa maonesho hayo uliofanyika katika viwanja vya SabaSaba Mjini Kibaha, Makamu wa Rais alisema udhamini huo unaunga mkono juhudi za serikali za kundeleza uanzishwaji wa viwanda ili kujenga taifa lenye uchumi wa kati unaochagizwa na viwanda.
“Naipongeza sana Benki ya CRDB kwa kudhamini maonesho haya huu ndio uzalendo tunaouzungumzia, wakati tunaelekea kwenye uchumi wa kati kwa kuifanya Tanzania kuwa ya viwanda, lazima tuwe wazalendo na benki ya CRDB wameanza.
“…Ni imani yangu mtaendelea hivi ili kutoa fursa kwa wajasiriamali wadogo, wakati na wenye viwanda kushiriki katika kubadilishana uzoefu na kuoneshana njia ya kuinua kipato kwa uchumi wa mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.
“Nimeridhishwa na washiriki nimeona kazi wanazofanya na kwa kweli tunapiga hatua, napenda kuwatia shime kwa hiki nilichokiona muendelee zaidi ya hapo,” alisema Makamu wa Rais, muda mfupi baada ya kutembelea mabanda ya washiriki wa maonesho hayo.
Aliitaka CRDB kupitia Mkurugenzi wake, Abdulmajid Nsekela kuendelea kuwakopesha wajasiriamali na wawekezaji wa viwanda huku akikumbuka mchango wa benki hiyo iliyodhamini pia uzinduzi wa Jukwaa la Uwezeshaji wa Wanawake kwa Mkoa wa Dar es Salaam na kuiomba ifanye hivyo kwa mikoa mingine ya Tanzania.
“Bado kuna fursa kubwa katika kuwakopesha wajasiamali, wakulima na wakinamama ili wawekeze katika ujenzi wa viwanda vidogo vidogo na kuongeza uzalishaji. Endelezeni ubunifu, ongezeni mtandao wenu, pitieni upya viwango vya riba ili viendane na hali halisi ya watanzania.
“Mkizingatia haya, mtakuwa mmetoa ahueni kubwa ya kiuchumi kwa watanzania walio wengi,” alisisitiza Makamu wa Rais.
Akizungumza wakati wa hafla hiyo, Mkurugenzi Mtendani wa Benki ya CRDB, Nsekela alisema benki hiyo inaunga mkono juhudi za serikali katika ujenzi wa Tanzania wa viwanda na maonesho hayo ni fursa adhimu katika kufungua milango ya masoko ya bidhaa za viwanda, jambo litakaloongeza kasi ya uzalishaji wa viwanda husika.
“Mheshimiwa Makamu wa Rais, kwa mwaka huu pekee, CRDB ilitoa mikopo ya zaidi ya Sh. Bilioni 433.5 katika kilimo ambayo ni asilimia 15 ya mikopo yote iliyotolewa na benki yetu. Hili linaifanya CRDB kuendelea kuwa kinara katika utoaji wa mikopo kwenye sekta ya kilimo.
“Vilevile, Benki imetoa mikopo ya zaidi ya Sh. Bilioni 60 katika biashara na sekta ya usafirishaji ili kurahisha kufikia masoko… sisi CRDB tunaamini kuwa ili viwanda vishamiri ni muhimu kusaidia ongezeko la uzalishaji wenye tija, usafirishaji na kufungua masoko,” alisema Nsekela.

No comments:
Post a Comment