HABARI MSETO (HEADER)


 


Breaking

October 21, 2018

TigoPesa, Google waunganisha malipo ya maudhui

NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI inayoongoza kwa maisha ya kidigitali nchini, Tigo, imekata kiu ya muda mrefu ya watumiaji wa simu janja ‘smart phone’ baada ya kuingia makubaliano na Google kuwapa wateja uwezo wa kulipia maudhui kutoka mtandao wa Google Play Store kwa njia ya TigoPesa. 

Awali, watumiaji wa simu hizo walikuwa wakitaka kulipia huduma za kununua muziki, cinema, apps au kusoma maudhui kwenye mtandao wa Google Play Store, walikuwa wakilazimishwa kufanya manunuzi kwa kutumia kadi ya benki.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Huduma za Kifedha ya Mtandao wa Tigo, Hussein Sayed, huduma hiyo inayowezeshwa na Bango, inahudumu kwa wateja milioni 7 wanaotumia huduma ya TigoPesa kulipia maudhui au ‘application’ yoyote inayopatikana Google Play Store kwa kutumia akaunti ya Tigo Pesa.

“Wateja wa Tigo wanaotumia simu janja za Android ama tablet, sasa wanaweza kufanya manunuzi ya moja kwa moja au malipo kwa njia ya kujisajili kupitia Play Store. Huduma hii inapatikana kwa njia rahisi na haraka mahali popote pale nchini kupitia TigoPesa. 
 
“Hii inawapa wateja wetu uwezo zaidi wa kupakua na kufurahia maudhui ya kimtandao kutoka Google Play Store, huku wakitumia mtandao wetu wa uhakika na wenye kasi ya juu zaidi wa 4.5G nchini,” alisema Sayed alisema jijini Dar es Salaam.

Suluhisho hilo linawawezesha wateja kufurahia huduma za manunuzi ya bidhaa na huduma walizozoea kwa kuunganisha matumizi ya Google Play na Tigo Pesa. Ili kukamilisha manunuzi mteja anatakiwa kufuata hatua za kawaida za kufanya manunuzi kwenye Play Store.

Kwa upande wake, Mahir Sahin, ambaye ni Mkurugenzi wa Google – Huduma za Android Barani Afrika, alisema: “Tuna furaha kubwa kuungana na Tigo kuzindua ubunifu huu utakaowezesha wateja wa Tigo Pesa kufanya malipo ya moja kwa moja kwenye Googe Play Store. 

“Hii itawezesha mamilioni ya Watanzania ambao hawana kadi za benki kufurahia huduma kamili za maudhui yanayopatikana kwenye Google Play,” alisdema Sahin.

Idadi kubwa ya Watanzania wanapenda kutumia simu zao za mkononi kufanya manunuzi ya huduma ya bidhaa, na sasa Tigo inawawezesha kununua maudhui wanayopenda zaidi kupitia huduma inayoongoza duniani ya Tigo Pesa.

No comments:

Post a Comment

Pages