*Ni baada ya kujengwa kwenye eneo la wazi na kuziba barabara
WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa
amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa
uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya
kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo
hilo.
Uzio
huo ambao mbali na kujengwa katika eneo la wazi lililotengwa kwa ajili
ya kuchezea watoto kwenye mtaa wa Mji Mpya kata ya Madukani pia umeziba
barabara ya tisa, hivyo kusababisha usumbufu mkubwa kwa watumiaji wa
barabara hiyo.
Waziri
Mkuu ametoa agizo hilo leo (Jumapili, Oktoba 21, 2018) wakati akiwa
katika ziara yake ya kikazi jijini Dodoma, ambapo alitembelea eneo hilo
na kuagiza libomolewe na lisalie kama inavyoonekana katika ramani na
aliyeuziwa atafutiwe eneo lingine.
“Huu
mji umejengwa kwa ramani, hamuwezi kubadili ramani kwa lengo la kumpa
mtu eneo. Kwa nini mmeziba barabara ya tisa na huu mji unatambulika kwa
barabara, sasa bomoeni hapa nataka barabara iendelee kutumika na eneo la
kuchezea watoto libaki wazi,”
Waziri
Mkuu amemuagiza mkurugenzi wa jiji ahakikishe wanayatumia maeneo ya
wazi kwa ajili ya kujenga sehemu za mapumziko ili kuwawezesha wananchi
kupata maeneo ya kupumzika mara wanapomaliza kufanya shughuli zao za
kikazi.
Amesema
ni vema jiji likatenga ardhi na kupima viwanja kwa ajili ya matumizi
mbalimbali yakiwemo ya biashara, makazi, taasisi, huduma za jamii,
viwanda pamoja na maeneo ya wazi kwa ajili ya mapumziko. “Msifanye
makosa kama yaliyofanyika Dar es Salaam.”
Kwa upande wake,
Mkuu wa Idara ya Ardhi na Mipangomiji wa jiji la Dodoma, Bw. Joseph
Mafulu alimuonyesha Waziri Mkuu ramani ambayo iliyotolewa na iliyokuwa
Mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu Dodoma (CDA) ambayo ilibadilisha
matumizi ya eneo hilo na kumpa muwekezaji.
Baada
ya Bw. Mafulu kuonesha ramani hiyo Waziri Mkuu alitoa ramani halisi ya
jiji la Dodoma ambayo inaonesha eneo hilo ni la wazi na ni mahususi kwa
ajili ya michezo ya watoto, hivyo alisisitiza kuwa litumike kama
ilivyokusudiwa na si vinginevyo.
Kufuatia
hatua hiyo, Waziri Mkuu aliwaonya watumishi wa halmashauri ya jiji la
Dodoma kutorudia makosa yaliyofanywa na CDA na kwamba jukumu lao ni
kuhakikisha wanayasahihisha makosa yaliyofanywa na mamlaka hiyo ili jiji
liweze kupangika vizuri.
Naye
Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Bw. Kunambi aliahidi kuyafanyia kazi
kikamilifu maelekezo yote yaliyotolewa na Waziri Mkuu na kesho
(Jumatatu, Oktoba 22, 2018) ataandika barua kwa Waziri wa Ardhi, Nyumba
na Maendeleo ya Makazi, Mheshimiwa William Lukuvi kwa ajili ya kufuta
hati ya eneo hilo na muwekezaji watampa eneo lingine.
Awali,Waziri
Mkuu alizungumza na watumishi wa halmashauri ya jiji la Dodoma, ambapo
aliwataka wabadilike na wasimamie vizuri rasirimali za umma pamoja na
kuwahamasisha na kuwasisitiza wananchi wafanye kazi kwa bidii ili
kufikia malengo maendeleo ya Taifa.
Waziri
Mkuu alisema mtumishi asiyeweza kufanya kazi kwa bidii anaweza kupata
matatizo kwa sababu Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa Rais Dkt.
John Magufuli imedhamiria kuwahudumia wananchi ipasavyo.
Kadhalika,
Waziri Mkuu aliwaagiza wakurugenzi wa halmashauri nchini pamoja na
mameneja wasimamie vizuri utendaji kazi wa watumishi mbalimbali katika
maeneo yao. Alisisitiza kuwa lazima watumishi wafanye kazi na matokeo
yaonekane.
Pia
Waziri Mkuu alifungua ofisi kuu ya kikosi cha Jeshi la Kujenga Taifa
(JKT) Makutupora na kisha alitembelea kiwanda cha kusindika zabibu cha
Alko Vintage na kukagua uzalishaji wa mvinyo katika kiwanda hicho
kilicho jijini Dodoma.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI MKUU,
S. L. P. 980,
41193 – Dodoma
JUMAPILI, OKTOBA 21, 2018.*Ni baada ya kujengwa kwenye eneo la wazi na kuziba barabara
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa
amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa
uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya
kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo
hilo. Pichani, mabati yakiwa yamezungushwa kwenye eneo hilo wakati
Waziri Mkuu alipolitembelea, Oktoba 21, 2018. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo. Pichani, Waziri Mkuu akimwonyesha Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi ( wapili kushoto) ramani ya jiji la Dodoma inayoonyesha matumizi sahihi ya eneo hilo, Oktoba 21, 2018.
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemuagiza Mkurugenzi wa jiji la Dodoma, Bw. Godwin Kunambi kubomoa uzio wa mabati uliojengwa kwenye eneo la wazi lililotengwa kwa ajili ya kuchezea watoto na kusitisha mara moja shughuli za ujenzi kwenye eneo hilo. Pichani, Waziri Mkuu akimwonyesha Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi ( wapili kushoto) ramani ya jiji la Dodoma inayoonyesha matumizi sahihi ya eneo hilo, Oktoba 21, 2018.




No comments:
Post a Comment