Mganga Mkuu wa Halmshauri ya Wilaya ya Newala, Judith Ringia, akizungumza na Waandishi wa Habari pamoja na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD), (hawapo pichani), kuhusu upatikaji wa dawa wilayani humo.
Ofisa Uhusiano wa MSD, Benjamini Masangya (kulia), akimuekeza Mganga Mkuu wa Wilaya ya Newala, Judith Ringia (wa pili kulia), namna ya kujiunga na mitandao ya kijamii. Wengine kutoka kushoto ni Afisa Huduma kwa Wateja wa MSD, Florida Sianga na Larisa Manyahi.
Kaimu Mganga Mfawidhi wa Kituo cha Afya cha Mkwedu, Emmanuel Bukuku, akizungumza na maofisa wa MSD, kuhusu upatikanaji wa dawa.
Wagonjwa wakisubiri matibabu katika Kituo cha Afya cha Mkwedu.
Mkazi wa Kijiji cha Makukwe, Muksini Faraji akizungumzia upatikanaji wa dawa katika Kituo cha Afya cha Mkwedu.
Mtunza Dawa wa Kituo cha Afya cha Mkwedu, Joseph Kibusi akitoa maelezo ya utunzaji wa dawa kwa maofisa wa MSD.
Mwonekano wa Jengo la Kituo cha Afya cha Mkwedu.
Mganga Mfawidhi wa Zaanati ya Mnali, Masanja Masunga, akizungumzia upatikanaji wa dawa na mafanikio ya utumiaji wa kondom.
Maofisa wa MSD wakizungumza na wagonjwa waliofika kutibiwa Zahanati ya Mnali.
Na Dotto Mwaibale, Newala
UELIMISHAJI wa matumzi ya mipira ya kiume (kondomu) katika Kijiji cha Mnali kilichopo Halmashauri ya Wilaya ya Newala DC kumesaidia kupunguza maambuki mapya ya Ukimwi.
Hayo yamebainishwa juzi na Mganga Mfawadi wa Zahanati ya Mnali Masanja Masunga wakati akizungumza na waandishi wa habari pamoja na maofisa wa Bohari ya Dawa (MSD) ambao wapo katika ziara ya kutembelea wateja wao na kujua changamoto zao.
"Matumizi ya kondomu hapa kijijini kwetu ni makubwa baada ya kutoa elimu kwa jamii ya matumizi yake hivyo yamesaidia sana kupunguza maambuki ya ukimwi" alisema Masunga.
Akizungumzia upatikanaji wa dawa katika zahanati hiyo alisema dawa zote muhimu 30 zinapatikana na kuwa pale wanapokuwa na upungufu na wakachelewa kuzipata kwa wakati wamekuwa na kawaida ya kukopesha na zahanati za vijiji jirani ili wananchi wasikose huduma.
Alisema zahanati yake licha ya kuhudumia vijiji takriban tisa inahudumia pia wananchi wengine kutoka vijiji jirani ambao wanafuata huduma katika zahanati hiyo lakini kutokana na kuongeza oda ya dawa kunakuwa hakuna changamoto ya hukosefu wa dawa.
Masunga alitaja vijiji anavyo vihudumia kuwa ni Mapinduzi, Chiule, Mnali, Mtopwa, Mkupeti, Chilondolo, Chikunda, Ngongo na Nanda na kuwa wagonjwa wanaopata huduma ni kati ya 20 hadi 70 kwa siku.
Mganga Mkuu wa Wilaya ya Newala, Judith Ringia alisema katika wilaya hiyo maambukizi mapya ya ukimwi ni asilimia 1.7 na kuwa magonjwa ya zinaa yanayosumbua wananchi ni kisonono na kaswande.
Akizungumzia upatikanaji wa dawa Ringia alisema kutokana na kuwepo kwa ushirikiano mzuri na MSD dawa zinapatika kwa wakati wote hadi kufikia asilimia 97.9.
Kaimu Mganga wa Kituo cha Afya cha Mkwedu, Emmanuel Bukuku alisema katika kituo hicho upatikaji wa dawa muhimu ni asilimia 100 na kuwa huwa wanazipata kwa wakati kutoka MSD na kuwa kwa siku huwa wanahudunia wagonjwa 40 hadi 50 kutoka katika vijiji vya Mkwedu, Tengalanga, Mnyambachi, Chiuta na Makule.
Mkazi wa Kijiji cha Makukwe, Muksini Faraji alisema kila anapofika kutibiwa katika kituo hicho cha afya anapata ushirikiano mzuri na hajawahi kukosa dawa.
Mkazi wa Kijiji cha Mtopwa, Karim Kazumali alisema yeye na familia yake wanatibiwa katika Zahanati ya Mnali na kuwa hawajawahi kukosa dawa pale wanapokwenda kutibiwa hivyo anaishukuru serikali kwa kuboresha huduma za afya.
Ofisa Uhusiano Mkuu wa MSD, Etty Kusiluka alitoa mwito kwa vituo vya afya, zahanati na Hospitali mkoani humo kujiunga na mfumo maalum wa kieletroniki utakao wasaidia kujua upatikanaji wa taarifa muhimu za upatikanaji wa dawa, vifaa tiba na vitendanishi vya maabara na bei zake, taarifa za akaunti zao na taratibu za maombi ya bidhaa wanazo hitaji kutoka MSD.
Alisema mfumo huo unajulikana kama“MSD-Customer Portal” unaweza kutumika na wateja wake popote walipo nchini na kuwaondolea usumbufu waliokuwa wakiupata awali wakati wakuagiza dawa, ambapo ili walazimu kusafiri ofisi za Kanda ya MSD inayowahudumia au kupiga simu ili kupata taarifa hizo na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment