HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

November 24, 2018

Milioni 10 za Tigo Jigiftishe zaenda kwa mkazi wa Changanyikeni Dar

Mkazi wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam, David Mmuni (katikati), akipokea mfano wa hundi ya  Sh. Mil. 10 alizoshinda katika promosheni inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo inayotoa zawadi za hadi shilingi milioni 50 kwa wateja watakaotumia huduma za mtandao huo katika msimu wa Sikukuu na Mwaka Mpya. Kulia ni Meneja wa Tigo, Kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa na kushoto ni Mkuu wa Huduma za Tigo Pesa, James Sumari. (Na Mpiga Picha Wetu).
 Meneja wa Huduma za Tigo Pesa, James Sumari akitoa maelezo kuhusu promosheni ya Jigiftishe na Tigo inayotoa zawadi zawadi sita za shilingi milioni moja kila siku, Milioni 10 kwa wiki na zawadi nono za hadi Sh. Mil. 50 kwa wateja watakaotumia huduma za kampuni hiyo katika msimu wa Sikukuu na Mwaka Mpya. Hii ilikuwa katika hafla ya kumakabidhi zawadi ya TSH 10 millioni mshindi wa wiki hii katika promosheni hiyo, David John Mmuni wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa akitoa maelezo kuhusu promosheni ya Jigiftishe na Tigo inayotoa zawadi zawadi sita za shilingi milioni moja kila siku, milioni 10 kwa wiki na zawadi nono za hadi Sh. Mil. 50 kwa wateja watakaotumia huduma za kampuni hiyo katika msimu wa Sikukuu na Mwaka Mpya. Hii ilikuwa katika hafla ya kumakabidhi zawadi ya TSH 10 millioni mshindi wa wiki hii katika promosheni hiyo, David John Mmuni wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam.

Baadhi ya wakazi wa eneo la Manzese jijini Dar es Salaam wakifuatilia hafla ya kukabidhi zawadi ya Sh. Mil. 10 kwa mshindi wa wiki wa promosheni ya Jigiftishe na Tigo, David John Mmuni ambaye ni mkaazi wa Changanyikeni, Dar es Salaam. 

Na Mwandishi Wetu 

MKAZI wa Changanyikeni jijini Dar es Salaam David John Mmuni, jana alikabidhiwa zawadi ya fedha taslimu shilingi milioni 10 baada ya kuibuka mshindi wa wiki katika promosheni inayoendelea ya Jigiftishe  inayoendeshwa na kampuni ya Tigo.

Mmuni ambaye anachangamoto ya kiafya ambayo iliyomfanya ashindwe kuzungumza, alionekana akiwa na uso wenye furaha huku akisaidiwa na ndugu yake Oscar John Mmuni kuelezea alivoweza kushinda fedha hizo.

Oscar aliwaambia waandishi wa habari katika hafla ya kumkabidhi zawadi yake iliyofanyika jijini Dar es Salaam kuwa,  wakati ndugu yake  anapigiwa simu ya kufahamisha  ameibuka mshindi, walikuwa katika Hospitali ya KCMC mjini Moshi ambako aalikuwa akiendelea kupata matibabu.

Alisema ndugu yake, alikuwa akinunua kifurushi cha data cha shilingi elfu mbili kila siku kwa kuwa sehemu walipofikia hapakuwa na Televisheni na hivyo alitumia simu yake kuangali Televisheni kwa nia ya mtandao.

‘David hakuweza kupokea simu kutokana na kuwa ni mgojwa na nilipokea kwa niaba yake. Nipoambiwa kuwa ameshindwa milioni 10 kutoka Tigo ilikuwa vigumu kuamini kwa kuwa siku hizi kuna utapeli mwingi na nilichokifanya nilirekodi kila kitu,” alisema.

Hata hivyo anasema baada ya kupata simu nyingine kadhaa kutoka kwa wafanyakazi wa Tigo aliamini na kuishukuru kampuni ya Tigo kutokana nafedha hizo ambazo zitasaidia matibabu ya ndugu yake.

Akizungumza wakati wa kumkabidhi zawadi, Meneja wa Huduma za Tigo Pesa, James Sumari  alisema kupitia promosheni ya Jigiftishe, tayari washindi 70 wamejishindia shilingi milioni moja, huku milioni 280 zikisubiri washindi wengine 280.

Sumari alisema zawadi ya milioni 10 ambayo hutolewa  mwishoni mwa wiki kwa mshindi mmoja, itakwenda kwa washindi wengine watano huku zawadi kubwa ya milioni 50,25 na 15 ikisuburi washindi mwisho mwa promosheni ambao ni tarehe 30 Desemba.

Promosheni hiyo ya kipekee ya ‘JIGIFTISHE’ kutoka Tigo katika msimu huu wa Krismasi na Mwaka Mpya itawafanya zaidi ya wateja 450 kuwa mamilionea ndani ya siku 45, kutokana na kutumia huduma za Tigo pekee. Ni rahisi na hakuna kujiunga kwenye promosheni hii.

Ili kujitengenezea nafasi ya kushinda mamilioni, mteja wa Tigo anatakiwa  kuweka  pesa kwenye akaunti yake ya Tigo Pesa, kuongeza salio au kununua simu janja kwenye maduka yote ya Tigo au kutumia huduma zozote za Tigo katika kipindi hiki cha sikukuu.

Kila muamala atakaofanya mteja,utampa nafasi moja ya kushiriki katika droo, na wateja wanaweza kutazama nafasi zao za kushinda kwa kupiga *149*22#. Kadri unavyofanya miamala zaidi ndivyo unavyojiongezea nafasi za kushinda.

No comments:

Post a Comment

Pages