Mshindi wa zawadi ya Sh. Mil. 10 katika
Promosheni ya Tigo Jigiftishe, Jane Jisandu (wa pili kushoto), akifurahia mfano wa
hundi kutoka kwa Mkurugenzi wa Tigo Kanda ya Pwani, Joseph Mutalemwa (wa pili kulia). Wanaoshuhudia wa kwanza kushoto
ni mtangazaji wa Radio Clouds FM, Mina Ally na wa kwanza kulia ni
Deogratius David kutoka Tigo.
Mshindi wa zawadi ya Sh.Mil. 10 katika
Promosheni ya Tigo Jigiftishe, Jane Jisandu (wa tatu kushoto), akiwa katika picha ya pamoja na washindi
wa shilingi milioni moja moja na wafanyakazi wa Tigo muda mfupi baada ya
kukabidhiwa zawadi yake Kivule jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki. (Na Mpiga Picha Wetu).
Na Mwandishi Wetu
Mkazi wa Kivule jijini Dar es Salaam Bi Jane Jisandu,
ameibuka mshindi wa zawadi ya wiki ya shilingi milioni kumi katika promosheni
inayoendelea ya Jigiftishe na Tigo.
Jane anakuwa mshindi wa tano wa zawadi ya
shilingi milioni kumi baada ya David Mmuni, Iyaka Muinga wote wa Dar es
Salaam, Mbwana Mbela mkazi wa wMpwapwa
mkoani Dodoma na Flora Somba wa Morogoro.
Akizungumza
muda mfupi baada ya kukabidhiwa zawadi yake Kivule jijini Dar es Salaam, Jane
alisema zawadi hiyo ni muujiza na kuongeza kuwa itasaidia kuokoa maisha ya
mwanaye ambaye anatakiwa kwenda India kwa ajili ya matibabu.
“Kwangu huu ni muujiza mkubwa sana. Nina mtoto
mgonjwa na ambaye nimeambiwa anaweza kutibiwa lakini mpaka nchini India. Gharama
za matibabu yake ni kubwa, nilikuwa nikiwaza wapi ningepata fedha za matibabu
lakini Mungu amenitendea muujiza kupitia Tigo, naishukuru Tigo kwa kuokoa
maisha ya mwanangu,” alisema.
Jane alisema
amefanikiwa kushinda zawadi hiyo baada ya kuwa antumia huduma za Tigo kama
kuweka kuma wa maongezi, kununua vifurushi mbali mbali pamoja na kutuma pesa
kwa njia ya Tigo Pesa huku akiwataka watu kutumia huduma za Tigo ili kujishidia
zawadi za fedha taslimu.
Akimkabidhi
zawadi kwa mshindi wa shiligi milioni kumi na wengine wa shilingi milioni moja
moja,Mkurugenzi wa Tigo kanda ya Pwani Joseph Mutalemwa alisema anayofuraha
kuona zawadi za fedha zinazotolewa katika Promosheni ya Jigiftishe zinagusa na
kubadilisha maisha ya wateja wa Tigo
Mutalemwa aliwataka wateja wa Tigo kuendelea
kutumia huduma za kampuni hiyo ili kujishindia zawadi za fedha taslimu na
kuongeza kuwa zawadi za fedha bado ni nyingi ikiwa ni pamoja na zawadi kubwa za
shilingi milioni 50,25 na 15 anbazo zitaolewa mwishoni mwa Promosheni.
No comments:
Post a Comment