NA JOHN MARWA
WAANDISHI wa Habari nchini wameaswa kufanya kazi
kwa kufuata misingi ya taaluma ya habari pasipo kuonea wala kuogopa mamlaka
yoyote katika kutekeleza majukumu yao
kwani wao ni mitume wa Mungu kueneza habari.
Hayo yamezungumzwa na viongozi wa dini kwenye
Semina ya jukumu la Mwanahabari katika jamii yake lililofanyika leo jijini Dar
es Salaam.
Akizungumza katika Semina hiyo Sheikh Hemed Jalala
amesema mwandishi mzalendo ni yule anayeitakia jamii yake kuendelea na sio
kuludi nyuma.
“Mwandishi mzalendo ni yule anayeitakia jamii yake
kuendelea na si kuludi nyuma, lakini pia uhuru wowote una mipaka yake ni vema
kama waandishi kutambua hilo.
“Jukumu la wanahabari
katika jamii ni kubwa kuliko inavyochukulia, kazi ya uanahabari ni kazi ya
Manabii na Mitume wa Mungu,”alisema Sheikh Jalala.
Akizungumza kwenye semina hiyo mwakilishi wa mgeni
rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dk. Abbas Hassan kwa niaba ya Waziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe alisema wanahabari
wafanye kazi kwa kuzingatia maadili ya kazi yao pasipo kwende kinyume kwa
maslahi ya Taifa na jamii kwa ujumla.
“Kitaaluma mwanahabari kuna misingi ya kuzingatia
unapo andika habari an hii wote tumeisoma hivyo basin in jukumu la kufanya kazi
kwa kuzingatia misingi hiyyo sambamba na Sheria za nchi na zile za mikataba ya
kimataifa ambayo Taifa lilingia pasipo kuogopa wala kuonea upande wowote.
“Mnayo haki ya kukusoa yale amabayo ni ya kweli
lakini pia mnayo haki ya kusifia yale amabyo ni mema katika jamii iwe yamefanya
na Serikali ama taasisi nyingine,”alisema Abbas.
Nae Mkurugenzi wa Tanzania Christian Outreach
Ministries Rev. Banza Suleiman aliwataka viongozi wa dini kujenga utamaduni wa
kuhubiri mamabo amabayo yanalinda utamaduni wa nchi ili wanahabari waweze
kuwafikishia watanznia.
Kwa upande wa Mkuu wa kitengo cha Habari Bakwata waandaji wa Semina hiyo Harith Mkusa amesema anachokifanya
mwanahabari ni kitukufu mbele za mwenyezi Mungu.
“Kazi mnayoifanya ni kazi takatifu licha ya kuwepo
wachache wanaokwenda kinyume, manapaswa kuthaminiwa, kulindwa kwa maslahi ya
Taifa,”alisema Mkusa.
Nae mwenyekiti wa Chama cha Waaandishi wa Habari
Wanawake nchini (TAMWA) Eda Sanga alisema nafasi ya wanawake katika tasnia ya
habari inapaswa kuheshimiwea na wanawake kuewa haki sawa katika bnafasi nyeti
za kiuongozi ndani ya vyombo vya habari.
Huku Mwenyekiti wa wamiliki wa mitandao ya kijamii
‘blog’ Joackim Mushi amesema kama watumiaji wa mitandao yab kijamii na jamii
ikiitumia kwa matuzi chanaya itakuwa na msaada mkubwa katika maendeleo ya jamii
nzima.
Sheikh Hemed Jalala
akizungumza katika Semina iliyoandaliwa na Jumuiya ya Waislamu Shia Ithnsheria Tanzania (T.I.C) ikishirikiana na Kitengo cha Maqasiliano Mawasiliano ya Umma, Ofisi ya Mufti wa Tanzania (BAKWATA).
Mgeni rasmi Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo Dk. Abbas Hassan(katikati waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment