Mkurugenzi
Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela akimweleza
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia),
changamoto zinazoikabili Mamlaka hiyo, wakati alipotembelea kukagua miundombinu
mbalimbali kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) akimsikiliza Msimamizi Kitengo cha
Mitambo, Bw. Gregory Kosamu (wa pili kushoto) aliyekuwa akielezea mifumo ya
Kiyoyozi ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA). Watatu
kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw.
Roichard Mayongela na kushoto ni Kaimu Meneja Matengenezo na Huduma za
Kiufundi, Bi. Diana Munubi.
Madereva wanaotoa huduma ya usafiri wa taxi
katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA), wakizungumza
na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alipokuwa
akikagua miundombinu ya Kiwanja hicho jana.
Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Isack Kamwelwe akizungumza na
Menejimenti na Waandishi wa Habari baada ya kufanya ziara ya kukagua
miundombinu ya Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jana.
Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw.
Richard Mayongela.
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na
Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe (kulia) jana akizungumza na Wafanyakazi wa
Kampuni ya inayotoa huduma kwa abiria na mizigo ya Swissport Tanzania, Bi.
Sarah Mlawa (kushoto) na Fliora Temba, alipokuwa akikagua miundombinu ya
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Raia wenye asili ya Asia kuanzia kulia Bi. Amina
Alblai, Bi. Amata Zavery na Bw. Aunali Zavery wakimsikiliza Waziri wa Ujenzi,
Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe alipofanya ukaguzi kwenye
Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) jana. Kushoto ni
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Richard
Mayongela. (PICHA NA MAMLAKA YA VIWANJA
VYA NDEGE TANZANIA (TAA).
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
xxxxxxxxxxxxxxxxxxxx
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya
Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Bw. Richard Mayongela, ameahidi kufanya Maboresho
makubwa katika Miundombinu ya Viwanja vya Ndege Tanzania na katika kuhamasisha kasi
ya utendaji ya wafanyakazi katika Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania.
Hayo ameyazungumza mbele ya
Waziri wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhandisi Isack Kamwelwe katika
mkutano na waandishi wa habari baada ya kufanya ukaguzi wa miundombinu katika
jengo la abiria la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA).
Awali Waziri Kamwelwe
alianzia ziara yake Katika Kiwanja cha Ndege cha Songwe na kubaini kwamba njia
ya kuruka na kutua ndege imejegwa chini ya kiwango na mkandarasi lakini pia
alipotua JNIA alibaini pia baadhi ya changamoto.
Kufuatia hatua hiyo Waziri
Kamwelwe ametoa maagizo kwa TAA kwamba kuanzia Januari mwakani kuwe na
mabadiliko katika namna ya utendaji.
“Nawaomba ndugu zangu kuanzia
Januari mwakani mbadilike na kama mtu hata badilika basi tutamtoa. Malalamiko
ya watu mimi nayapokea na ninayafanyia kazi, kwa maana hiyo ni vyema pia
muyafanyie kazi”, alisema Mhandisi Kamwelwe.
Bw. Mayongela akizungumza kwa
niaba ya Menejimenti katika kikao hicho amebainisha kwamba ujio wa Waziri ni
changamoto kwa watendaji wote wa TAA kila mtu ajithimini katika kipindi hiki na
kukaa tayari kwa ajili ya maboresho makubwa na utendaji wa kasi wa Mamlaka.
“Kwa niamba ya Wenzangu
tunakuahidi kwamba kuanzia januari mwaka unapoanza tutajitahidi kufanya kazi
kwa weledi na kwa uadilifu Mkubwa. Kwa upande wa Kiwanja cha Ndege cha
Kimataifa cha Julius Nyerere kuendelea kulalamikiwa kwa kwa mambo madogo madogo
ya kiutendaji haioendezi na ni aibu kwetu, mimi mwenyewe kama mtendaji mkuu
nitachukua hatua na kuhakikisha kwamba tunakipa hiki kiwanja kipaumbele”.
Hatahivyo, Waziri Kamwelwe
amewatakia watanzania wote heri ya sikukuu za mwisho wa Mwaka na kuwaasa kwamba
watumie hii nafasi kujiandaa ili kuja kufanya kazi vizuri mwakani. (IMETOLEWA NA KITENGO CHA MAHUSIANO CHA
MAMLAKA YA VIWANJA VYA NDEGE TANZANIA (TAA).
No comments:
Post a Comment