Kauli hiyo ilitolewa na
Katibu Mkuu wa Chama cha Wananchi CUF Maalim Seif Shariff Hamad wakati
akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza kikao hicho cha siku tatu
kilichofanyika Zanzibar kwa niaba ya vyama hivyo.
‘’Kama vyama vya
siasa vyenye uhalali na uratibu wa uliowekwa rasmi kikatiba, tunatangaza rasmi
namna ya kufanya mikutano yetu ya hadhara katika kila kona ya nchi yetu’’
alieleza Maalim Seif.
Alieleza hawatoruhusu
katazo haramu ambalo alisema linakwenda kinyume na sheria za nchi na kudai
haliwezi kuzuia kazi zao.
Aliwataka wanachi
pamoja wanachama wote wa vyama sita, wakati ni sasa wa kuondoa hofu na kuunga
mkono vyama vyao ili kulinda Demokrasia.
‘’Hatupaswi kuwa waoga
hata kidogo na hatupaswi kujisalimisha katika kudai haki zetu kama mtu mmoja au
kikundi, lazima tupeleke ujumbe huu wa uhuru na Demokrasia kwa viongozi wenzetu
wote’’ alieleza.
Sambamba na hilo
waliwatangaza viongozi wa vyama vya siasa Freeman Mbowe na Esther Matiko ambao hadi sasa wako mahubusu
kuwa ni Wafungwa wa Kisiasa na kueleza kuwa tangazo hilo halitofutwa mpaka pale
watakapoachiwa.
‘Tutapambana kwa nguvu
zote kuhakikisha wafungwa wote wa
Kisiasa, nchi nzima wanapewa nafasi ya
kupata haki katika mfumo ulio huru mbele ya mahakama na macho ya watu’’
alieleza Maalim Seif.
Mwenyekiti wa Chama cha
UMMA Hashim Rungwe alisema hawawezi kumruhusu mkandamizaji wa siasa aendelea
kuwakandamiza wanachi na demokrasi na kueleza sasa basi.
‘’Lazima tuwaeleze
wananchi wakatae utawala huu wa kibabe kwani ndio uliopomorosha maisha yao’’
alifafanua Rungwe.
Alieleza kuwa
Demokrasia ina gharama na wakati ukifika watawaeleza nini watafanya katika
kupiga viota uvunjwaji wa Demokrasia.
Akizungumza katika
mkutano huo ambao ulitoka na tamko la Azimio la Zanzibar Mwenyekiti wa ANSSRA Jemse
Mbatia alisema hali iliyopo sasa ni kutokana na ubinafsi ya utawala uliopo.
Alieleza kuwa ubinafsi
huu ndio uliopelekea maisha ya watu kubadilika na kuwaona wengine ndio walio na
haki hapa nchini.
Kwa upande Wa Zanzibar vyamna
hivyo vilieleza kuwa hawaitambui Serikali ya Mapinduzi inayo Ongozwa Dr. Ali
Muhammed Shein na kuita ni serikali haramu kutokana kile walichodai kupora
ushindi wa CUF mwaka 2015.
Akizungumzia baadhi ya
wabunge na Madiwani waliohama vyama na kujiunga CCM Waziri Mkuu wa zamani Fredric Sumaye alieleza
kuwa viongozi hao hawakuhama bure na wamenda kufanya biashara ya kisiasa.
‘’Unapoona wabunge na
viongozi wa upinzani wanahamia chama tawala ujue chama tawala kimefika mwisho
kutawala katika nchi, na hapa ni dhahiri CCM wamefikia mwisho kutawala Tanzania’’
alieleza Sumaye
No comments:
Post a Comment