Mkuu
wa Taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Kubilag akiongozwa na
kijana wa skauti mara baada ya kuwasili katika viwanja vya shule ya
sekondari Kibwegere alipokwenda kukabidhi visima vitatu kwa shule tatu
tofauti zilizopo katika eneo hilo, Kibamba jijini Dar es Salaam.
Skauti
wakionyesha uwezo wao katika mchezo wa sarakasi wakati wakitumbuiza
jana, wakati wa uzinduzi wa visima vitatu vilivyochimbwa na wahisani wa
taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi
wa Shule ya Msingi Kibwegere wakitumbuiza wakati wa uzinduzi wa visima
vitatu vilivyochimbwa na wahisani wa taasisi isiyo ya kiserikali ya
Time to help, jijini Dar es Salaam.
Skauti
wakionyesha uwezo wao katika mchezo wa sarakasi wakati wakitumbuiza
jana, wakati wa uzinduzi wa visima vitatu vilivyochimbwa na wahisani wa
taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari ya Kibweheri, Alexandra Ngonyani (kulia),
akizungumza jana wakati hafla ya uzinduzi wa visima vitatu
vilivyochimbwa na wahisani wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to
help, jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni mkuu wa shirika hilo,
Kubilag Talu
Mlezi
wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Remziye Talu
(katikati), akizindua kisima cha maji katika shule ya sekondari
Kibwegere jana, kilichojengwa na taasisi hiyo, Kibamba, Dar es Salaam.
Wanaoshuhudia wa kwanza kulia ni Naibu Mkuu wa Shule ya Sekondari
Kibwegere, Halima Mgaya na Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibweheri,
Alexandra Ngonyani.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Kibweheri, Alexandra Ngonyani (kushoto) na Mlezi
wa taasisi isiyo ya kiserikali ya Time to help, Remziye Talu wakifungua
bomba la maji ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa akizindua kisima cha maji
katika shule ya sekondari Kibwegere jana. Kulia anayeshuhudia ni Naibu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya.
Mwalimu
Mkuu Msaidizi wa Shule ya Msingi Kibwegere (wa kwanza kushoto), Mkuu wa
Shule ya Sekondari Kibweheri, Alexandra Ngonyani na Naibu Mkuu wa Shule
ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya, wakimshukuru mlezi wa taasisi ya
Time to help, Remziye Talu (kulia) mara baada ya uzinduzi wa kisima
kilichojengwa na taasisi hiyo katika shule ya sekondari Kibwegere.
Mkuu
wa Shule ya Sekondari Kibweheri, Alexandra Ngonyani (kushoto), na Naibu
Mkuu wa Shule ya Sekondari Kibwegere, Halima Mgaya (wa pili kushoto),
wakimshukuru mlezi wa taasisi ya Time to help, Remziye Talu (kulia) mara
baada ya uzinduzi wa kisima kilichojengwa na taasisi hiyo katika shule
ya sekondari Kibwegere.
No comments:
Post a Comment