HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 18, 2019

Blockbonds, Benki I&M wazindua SPENN


Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya I&M Tanzania, Baseer Mohammed, akizungumza katika uzinduzi wa App ya SPENN uliofanyika jijini Dar es Salaam, ambapo mteja wa benki hiyo anaweza kufanya miamala mbalimbali bure kwa kufungua akaunti binafsi au ya biashara. Kulia ni Meneja Mauzo wa Spenn Tanzania, Chunsi Ngogomba na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Blockbonds, Jens Glaso. (Picha na Francis Dande).
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Blockbonds, Jens Glaso, akizungumza katika hafla hiyo.

Meneja Mauzo wa Spenn Tanzania, Chunsi Ngogomba, akifafanua jambo.

Ofisa Mtendaji Mkuu wa Blockbonds, Jens Glaso, akizungumza katika hafla hiyo.
Maofisa wa Benki ya I&M wakiingia katika APP ya SPENN. 
 Wadau wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya maofisa wa Benki ya I&M wakifuatilia uzinduzi huo.
 Uzinduzi ukiendelea.
Wadau wakiwa katika uzinduzi huo.

Baadhi ya maofisa wa Benki ya I&M Tanzania wakiwa katika uzinduzi huo.

Uzinduzi ukiendelea.

Baadhi ya maofisa wa Benki ya I&M Tanzania wakifuatilia uzinduzi wa APP ya SPENN.
 
Kuchukua taswila.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya I&M Tanzania, Baseer Mohammed, akinunua bidhaa kwa kutumia huduma mpya ya SPENN katika moja ya maduka eneo la Kariakoo jijini Dar es Salaam.

Meneja Masoko na Mawasiliano wa Benki ya I&M Tanzania. Emmanuel Kiondo, akizungumza na waandfishi wa habari wakati wa uzinduzi wa APP ya SPENN.

Picha ya pamoja.

Picha ya pamoja.

Baadhi ya mapfisa wa Benki ya I&M Tanzania wakipata viburudisho baada ya uzinduzi wa APP ya SPENN.


NA MWANDISHI WETU

KAMPUNI ya Blockbonds, yenye makao makuu yake nchini Norway kwa kushiriklana na Benki ya I&M Tanzania, wamezindua huduma mpya na bunifu yenye kuwezesha kufanya malipo bure, ijulikanayo kama SPENN.

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dar es Salaam, ambako kuanzia sasa, SPENN inakuwa huduma inayokuja kuhudumu kupitia Benki ya I&M, inayomuwezesha mteja kufanya miamala mbalimbali bure, ikiwamo kufungua akaunti binafsi na akaunti ya biashara.

Akizungumza wakati wa uzinduzi huo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa Blockbonds, Jens Glaso, hakusita kuelezea furaha yake kuingiza rasmi huduma hiyo katika soko jingine barani Afrika, baada ya kufanikisha kuizindua rasmi nchini Rwanda mwaka jana 2018.

Kwa mujibu wa Glaso, huduma ya SPENN imepokelewa vema nchini Rwanda, ambako hadi sasa ina watumiaji zaidi ya 130,000, ikiwa ni katika kipindi kifupi tangu ilipozinduliwa rasmi.

“Lengo Ietu ni kuhakikisha kwamba kila mmoja anapata fursa ya huduma za kifedha kupitia teknolojia yenye ubunifu wa hali juu. Kufanikisha upatikanaji wa huduma ya SPENN nchini Tanzania ni hatua kubwa sana katika kutimiza malengo yetu ya muda mrefu,” alisisitiza Glaso.

Kwa kupakua App ya SPENN bure, mtu yoyote anaweza kufungua akaunti ambaye haina gharama za uendeshaji, ambako kila mtumiaji anaweza kutuma na kupokea pesa, kufanya malipo katika maduka mbalimbali pamoja na kuweka na kutoa fedha katika tawi lolote la Benki ya I&M.

Vile vile huduma ya SPENN inakupa suluhisho la bure la kufanya biashara ya kuuza bidhaa na huduma kwa ufanisi kwa kukupa njia ya rahisi ya kupokea malipo bila kutumia fedha taslimu endapo mteja atajisajili kuwa mtumiaji wa SPENN Plus.

No comments:

Post a Comment

Pages