NA KENNETH NGELESI, MBEYA
MEYA
wa
Jiji la Mbeya Devid Mwashilinsdi ameongoza watumishi wa halmashauri ya jiji la
Mbeya kutembea kituo cha watoto yatima cha Malezi ya huruma Simike jijini Mbeya na
kutoa msaada wa maitaji vyakula,vinywaji na vifaa vya shule.
Akizungumza
wakati akikabidhi msaada mwishoni mwa wiki kwa mama mleza wa kituo hicho wa Anna Kasile, Meya
Mwashilindi alisema kuwa msaada huo umetolewa na watumishi wa Halmashauri hiyo
baada ya kuchangishana fedha na baaye wamenunua mahitaji kwa ajili ya watoto
wanao lelewa katika kituyo hicho.
‘Nitumie
fursa kuwashukuru watumishi wa Halmashauri ya jiji kwa kuamu kuchangishana pesa
na kununua mahitaji kwa ajili ya watoto
wetu wanao lelewa katika kituo hiki’ alisema Mwashilindi.
Mwasdhilinmdi
alibanisha baadhi ya vitu vilivyo tolewa na watumishi hao kuwa ni Daftari,
Msafuta ta kupikia,Sabuni ya Unga,Sabuni za mche, Mchele,Kuku,na Sukari na soda
na pesa taslimu elfu sh.40000/ kwa ajili ya kununulia maitaji mengine.
‘Pesa
hizi zimetoka mifukoni mwa hawa watumishi hivyo japo ni kidogo tunaomba upokee
na tunaamini vitaweza kuwa saidia vijana wetu’ aliongeza Mwashilindi
Akizungumza
mara baada ya kupokea msaada huo Mama Mlezi wa kituo hicho aliwashukuru
watumisahi kwa kujaliwa moyo moyo wa huruma na upendo na hatimaye wameweza
kuwakumbuka watoto wanao ishi katika mazingira magumu na hatarishi.
‘Nawashukuru
sana kwa msaada huu kwani inaonyesha ni jinsi mlivyo na moyo wa huruma na
upendo kwa watoto na niwasii muendelee moyo huo huo wa watu wenye mahitaji
maana hata maandiko yanatukumbusha atoaye kwa ukarimu hupokea kwa ukarimu
msiishie katika kityuo huiki bali hata vituo vingine’ alisema Kasile
No comments:
Post a Comment