Waziri wa Fedha na Mipango
Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango akiorodhesha baadhi ya hoja zilizowasilishwa na
Wafanyabiashara wa Sekta mbalimbali wakati wa kikao na Wafanyabiashara hao,
kilichofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa AICC mkoani Arusha,
Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki.
Na
Josephine Majura na Ramadhani Kissimba, WFM, Arusha
Waziri wa Fedha na
Mipango, Mhe.Dkt. Philip Isdor Mpango amezitaka Taasisi zote za Serikali
kutumia kikamilifu mfumo wa malipo wa Serikali wa kielektroniki (GePG), ili kutimiza
azma ya Serikali ya kudhibiti mianya ya upotevu wa fedha za Umma.
Dkt. Mpango ameyasema
hayo mwishoni mwa wiki wakati wa kikao cha wafanyabiashara wa sekta ya madini,
utalii, mahotel na viwanda wa Mkoa wa Arusha kilichofanyika katika ukumbi wa
Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC).
Akijibu hoja na
kutolea ufafanunuzi wa kero mbalimbali zilizowasilishwa na Wafanyabiashara hao,
Dkt. Mpango alisema Serikali ilishatoa maagizo kwa Taasisi zote za Serikali
kuwa malipo yote yafanyike kwa kutumia mfumo wa malipo ya Serikali, na endapo
itatokea Taasisi yoyote itashindwa kufanya hivyo itachukuliwa hatua za
kisheria.
“Serikali
iliziagiza Taasisi zote kuanza kutumia mfumo wa malipo ya Serikali ifikapo
mwezi Juni, 2019, na nina agiza kuanzia leo mwananchi yeyote asikubali kulipa
malipo yoyote yasiyotumia mfumo huu” alisisitiza
Dkt. Mpango.
Kwa upande wake,
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, anayeshughulikia Uwekezaji Mhe. Angela Kairuki alisema Serikali
inatambua mchango mkubwa unaotolewa na Sekta Binafsi katika kukuza uchumi wa
nchi, hivyo Serikali imekuwa ikifanya jitihada mbalimbali kuhakikisha kwamba
inaboresha mazingira ya ufanyaji biashara hapa nchini.
Mkutano huo uliandaliwa
na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, kwa lengo la kutatua kero
mbalimbali za Wafanyabiashara wa Mkoa huo, na kuhudhuriwa na Waziri wa Viwanda na Biashara Mhe. Joseph
Kakunda, Waziri wa Mambo ya ndani ya nchi Mhe. Kangi Lugola, Waziri wa nchi,
Ofisi ya Makamu ya Rais Mazingira Mhe. Januari Makamba, Waziri wa Ujenzi na
Uchukuzi Eng. Isack Kamwele, Naibu
Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe. Abdallah Ulega, Naibu Waziri wa Maliasili na
Utalii, Mhe.Constantine Kanyasu, na Naibu Waziri wa Vijana, Kazi na Ajira, Mhe.Anthony
Mavunde.
No comments:
Post a Comment