Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo cha Michezo Kahama, Hamis Mgeja akitazama moja ya jezi alizopokea kutoka kwa mbunge wa Kahama, Jumanne Kishimba kwaajili ya ligi ya soka kwa vijana chini ya miaka 20 inayoendelea wilayani Kahama.
Baadhi ya viongozi wa timu zinazoshiriki mashindano hayo wakiwa na vifaa walivyokanidhiwa na mbunge wa Kahama, Jumanne Kishimba.
NA MWANDISHI WETU, KAHAMA
MBUNGE wa Kahama, Jumanne Kishimba (CCM) amegawa vifaa vya michezo kwa timu 10 zinazoshiriki ligi ya soka kwa vijana chini ya miaka 20.
Vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya Sh. milioni 3.2 vilikabidhiwa kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini wa Kituo cha Michezo cha Kahama, Khamis Mgeja kwa niaba ya wadau wa michezo Wilaya ya Kahama, mkoani Shinyanga.
Ligi hiyo iliyoanza hivi karibuni inabeba kaulimbiu isemayo 'Mzazi kaa na mwanao, michezo ni utajiri na ajira.
Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo, Kishimba alisema ameguswa kwa kuwa michezo ni njia sahihi kwa vijana kuelekea kwenye utajiri.
"Natambua kwamba sasa hivi michezo hasa soka inanafasi sana duniani katika kuunganisha vijana na ajira. Soka lina wapenzi wengi ulimwenguni na watu wamewekeza huko.
"Tangu mwaka 2016 ninazisaidia timu za michezo mbalimbali na nitaendelea kufanya hivyo nikiamini kwamba vijana wanaoshiriki wanajiajiri na wanao uhakika wa kutajirika, ndio maana nasema michezo sio kitu cha kupuuza," alisema Kishimba.
Baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo, Mgeja alimshukuru Kishimba kwa kukubali ombi la wadau kusaidia michezo na kusema washiriki wa ligi hiyo na wafuatiliaji wake hawana itikadi za kusiasa, ukabila wala udini.
"Haya mashindano yalianza rasmi mwaka 2017 kwa timu za vijana chini ya miaka 17 na tutaendelea kuwahamasisha vijana washiriki zaidi katika hili.
"Baada ya mashindano haya tutaanzisha mengine ya vijana chini ya miaka 14 lengo ni kuhakikisha vijana wa rika tofauti wanashiriki michezo na kuimarisha umoja kati yao," alisema Mgeja.
Mratibu wa mashindano hayo, Shabani Nguno, alizitaja timu shiriki kuwa ni Kahama Herose Academy, Famhano FC, Michigan, Mnarani, Nyahanga, Kahama Rangers, Young City, Majengo, Mngole Nyasuni na Danglte FC.
"Zawadi zitakazotolewa kwa mashindi wa kwanza ni ng'ombe mkubwa, mshindi wa pili ni mbuzi na mshindi wa tatu ataondoka na jogoo," alisisitiza Nguno.
Kwa mujibu wa Nguno michezo hiyo inatarajia kumalizika Aprili mwaka huu.

No comments:
Post a Comment