HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 22, 2019

WAZIRI UMMY AWAPONGEZA WAWEKEZAJI VIWANDA VYA DAWA KIBAHA

Waziri wa  Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu akisaini kitabu cha wageni alipofika katika eneo linapojengwa Kiwanda cha Madawa cha Vista Pharma Ltd kilichopo Kibaha mkoani Pwani. (Picha na Francis Dande).
Waziri wa  Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu, akisalimiana na mwekezaji wa Kiwanda cha Madawa cha Vista Pharma Ltd,  wakati wa ziara yake ya kuangalia maendeleo ya viwanda vya kutengeneza dawa mkoani Kibaha.
Waziri wa  Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu (katikati), akifafanua jambo wakati alipofanya ziara katika Kiwanda cha Madawa cha Vista Pharma Ltd.
Mhandisi Basem Khader kutoka Kampuni ya Petra Construction waonajenga Kiwanda cha Vista Pharma akitoa maelezo kwa waziri wa afya juu changamoto wanazokabiliana nazo wakati wa ujenzi wa kiwanda hicho.
Moja ya majengo ya ofisi katika kiwanda cha Vista Pharma.
Kiwanda cha Vista Pharm kikiwa katika hatua za awali za ujenzi wake.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa Kiwanda cha Madawa cha Vista Pharma Ltd, Churchil Katwaza, akisoma taarifa za kiwanda hicho kwa Waziri wa  Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu.
Msafara wa Waziri wa  Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu, ukiwasiri katika eneo la uwekezaji la Kiwanda cha Madawa cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Limited (KPIL).
Waziri wa  Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu, akiangalia ramani ya ujenzi wa Kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Limited (KPIL).
Msimamizi wa Kiwanda cha Madawa cha KPIL, kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Dk. Muganyizi Kairuki, akitoa maelezo juu ya junzi wa kiwanda hicho kwa Waziri wa Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu.
Waziri wa Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu akiwa katika ziara ya kukagua maendeleo ya ujenzi wa Kiwanda cha Madawa cha Kairuki, kilichopo Kibaha mkoani Pwani.
Waziri akipata maelezo ya ujenzi wa Kiwanda cha Madawa cha KPIL.
Msimamizi wa Kiwanda cha Madawa cha Kairuki, kilichopo Kibaha mkoani Pwani, Dk. Muganyizi Kairuki, akizungumza na waandishi wa habari wakati wa ziara ya Waziri wa Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu (katikati), kutembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa viwanda vya dawa vya Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd (KPIL) na Vista Pharma Ltd.
Kutembelea eneo la kiwanda.
Waziri wa Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy  Mwalimu, akisaini kitabu cha wageni alipofika katika Kiwanda cha Madawa cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd.
Msimamizi wa Kiwanda cha Madawa cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd (KPIL), Dk. Muganyizi Kairuki akitoa taarifa ya ujenzi wa kiwanda hicho kwa Waziri wa Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy, alipofanya ziara katika kiwanda hicho.
Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Pwani akizungumza  wakati akimkaribisha waziri wa afya kuzungumza.
Waziri wa Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy, akitoa majumuhisho baada ya kutembelea viwanda vya kutengeneza madawa vya Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd na Vista Pharma mkoani Kibaha.
Waziri wa Afya, Ustawi  wa Jamii, Jinsia, Wazee  na Watoto, Ummy, akitoa majumuhisho baada ya kutembelea viwanda vya kutengeneza madawa vya Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd na Vista Pharma mkoani Kibaha.
Mbunge wa Kibaha Mjini akitoa neno kwa wawekezaji wa viwanda vya madawa.
Waziri Ummy akitoka katika moja ya majengo katika eneo la kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd.
Eneo la ujenzi wa kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd.
Waziri akiagana na Dk. Muganyizi Kairuki.
Waziri Ummy akiagana na Ofisa Mtendaji Mkuu wa Vista Pharma.
Waziri Ummy akitoka katika kiwanda cha Kairuki Pharmaceutical Industrial Ltd baada ya kumaliza ziara yake.
Picha ya pamoja.


NA MWANDISHI WETU

WAZIRI wa Afya, Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, amesema katika kila Sh. 100 ambayo Serikali inatumia kununua dawa nchini, Sh. 94 inapelekwa nje ya nchi kwa ajili ya ununuzi wa dawa hizo.

Waziri Ummy alisema hayo jana wilayani Kibaha, Pwani wakati wa ziara yake ya kutembelea na kuangalia maendeleo ya ujenzi wa Viwanda vya dawa ambavyo ni Kampuni ya Kairuki Pharmaceutical Industrial Limited (KPIL) na Vista Pharma Ltd.

Alisema fedha hiyo inayokwenda nje kwa ajili ya ununuzi wa dawa ni kubwa na ili kuikoa ni muhumu kwa wawekezaji kuendelea kuwekeza nchini hasa katika ujenzi wa viwanda vikiwemo vya dawa na vifaa tiba ambavyo ndivyo vinapewa kipaumbele na serikali.

"Changamoto tunayopitia Serikali mbali na kwamba tunatumia fedha nyingi katika uagizaji wa dawa, bado dawa hizi zinachelewa kufika, Bohari ya Dawa (MSD) imekuwa ikiagiza dawa nje ya nchi na dawa hizo hukaa takribani zaidi ya miezi sita ndio zinaingia nchini, jambo hili ufanya upatikanaji wa dawa usiwe rahisi. “Hivyo tunaposema upo umuhimu wa ujenzi wa viwanda vya dawa tunamaanisha," alisema.

Alisema ujenzi wa viwanda nchini utasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza gharama za uagizaji wa dawa hizo nje ya nchi, gharama za upatikanaji wa dawa nchini kushuka na kuokoa fedha zinazonunulia dawa hizo.

"Kati ya wadau 72 wa masuala ya afya nchini walioomba kujenga viwanda vya dawa hapa nchini, ni nane mpaka sasa ndio wameanza kujenga na kati ya hao sita viwanda vipo Kibaha.

“Hii inaonyesha ni kwa namna gani viwanda hivi vikikamilika vitakavyozalisha dawa zenye ubora zaidi na kuhakikisha tunaokokoa fedha za nje tunazozitumia katika kununua dawa," alisema na kuongeza "Kwa mwaka huu wa fedha serikali imetenga Sh. Bilioni 270 katika wizara yangu kutoka Sh. Bilioni 30, hivyo fedha za kununua dawa zipo wawekezaji wakazane wamalize haraka viwanda hivyo ili fedha hizi zibaki hapa nchini, " alisema.

Hata hivyo, alisema serikali itahakikisha inatengenza mazingira mazuri ya kurahisisha ujenzi wa viwanda unaenda sambamba na uimarishaji wa miundombinu ya umeme, maji na barabara.

Kwa Upande wake, Msimamizi wa Kiwanda cha Kairuki, Dk.Mganyizi Kairuki, alisema kiwanda chao kinatarajia kuanza uzalishaji wa dawa za maumivu na nyingine aina 10 ambazo ni za maji ifikapo mwakani.

Alisema mbali na uzalishaji wa dawa, kiwanda hicho pindi kitakapokamilika kinatarajia kutoa ajira za moja kwa moja 200 na zisizo za moja kwa moja 1,000.

"Zaidi ya Sh. Bilioni 38 zinatarajiwa kutumika katika ujenzi wa kiwanda hiki fedha ambazo ni mikopo kutoka benki, hivyo tunazidi kuziomba baadhi ya benki kukopesha maana suala hili limekuwa ni changamoto," alisema.

Naye Mwenyekiti wa Kampuni ya Bandari Pharmacy inayojenga kiwanda cha Vista Pharmacy, Churchill Katwaza, alisema kiwanda chao kinatarajia kuzalisha dawa sita ikiwemo ya kutuliza maumivu ya tumbo, kuongeza damu kwa wajawazito pamoja na inayotibu ushambulizi wa vidudu vya bakteria mwilini.

"Tutazalisha jumla ya vidonge milioni 702 kwa mwaka na takribani chupa milioni 32 za dawa ya maji zenye ujazo wa milimita 100,"alisema Katwaza.

No comments:

Post a Comment

Pages