HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

February 07, 2019

Total Tanzania Kuzindua Kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants)

Kampuni ya Mafuta ya Total Tanzania Limited itazindua kiwanda chake cha Vilainishi (Lubricants) kilichoko katika eneo la viwanda la Chang'ombe- Temeke, Dar es Salaam.
Uzinduzi wa kiwanda hiki, kutaifanya kampuni ya mafuta ya Total Tanzania kuwa ndio kampuni pekee ya kimataifa nchini Tanzania yenye kutengeneza vilainishi vyake yenyewe ambapo inatarajiwa itazalisha zaidi ya tani 15,000 za vilainishi kwa ajili ya soko la ndani ya nchi na ziada itauzwa nje nchi.
Kwa zaidi ya miaka 50 ya uwepo wake nchini Tanzania, Kampuni ya mafuta ya Total Tanzania ilikuwa ikiagiza vilainishi vyake kutoka nje ya nchi lakini kuanzia sasa, vilainishi hivyo vinatengenezwa humu humu nchini.
Uzinduzi wa kiwanda hiki, kutaifanya kampuni ya mafuta ya Total Tanzania Limited kuunga mkono kwa vitendo, mkakati wa rais Magufuli na serikali yake ya Awamu ya Tano katika ujenzi wa Tanzania ya Viwanda. Kiwanda hiki licha ya kuchangia katika maendeleo ya taifa kiuchumi na kitekinolojia, pia kitatoa nafasi za ajira kwa Watanzania.

No comments:

Post a Comment

Pages