Baadhi
ya wajasiriamali wadogo wadogo wakipata maelezo na wengine wakichukua
vitambulisho vya wajasiriamali katika eneo la Mkwajuni Wilayani Songwe.
Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Brigedia Jenerali mstaafu, Nicodemus Mwangela, akimpatia kitambulisho cha wajasiriamali wadogo wadogo mchimbaji mdogo wa madini katika Kijiji cha Saza, wilayani Songwe jana. (Picha na Ofisi ya Mkoa- Songwe).
Songwe, Tanzania
Wavuvi
na wachimba madini wadogowadogo wamepewa muda wa siku nane kuchukua
vitambulisho vitakavyo wawezesha kutambulika rasmi kama wajasiriamali wadogo
wadogo ili waweze kufanya shughuli halali za uzalishaji mali bila kusumbuliwa.
Mkuu
wa Mkoa wa Songwe Brig. Jen. (Mst) Nicodemus Mwangela ametoa maelekezo hayo
mapema wiki hii akiwa ziarani Wilayani Songwe ambapo ametembelea kambi ya
wachimbaji wadogo wa madini katika Kijiji cha Saza na wajasiriamali wa uvuvi
katika kambi ya sabasaba pembezoni mwa mto Rukwa.
Brig.
Jen. (Mst) Mwangela amesema, “mjasiriamali mdogomdogo unayefanya shughuli
yeyote halali inayokuingizia kipato na hulipi kodi TRA serikali inataka
kukutambua hivyo basi unatakiwa kuchukua kitambulisho ili usisumbuliwe”.
Aidha
amezitaka halmashauri za Mkoa wa Songwe kuhakikisha zinasimamia vizuri ugawaji
wa vitambulisho vya wajasiriamali wadogo ili kuepuka udanganyifu na kuhakikisha
kila mjasirimali anatambulika kwa kupata kitamblisho hicho.
Naye
Afisa Kodi Kutoka Mamlaka ya Mapato nchini TRA Omary Iddi amesema wajasiriamali
wadogowadogo ambao kipato chao kwa siku wanapata chini ya shilingi milioni nne
kwa mwaka wanapaswa kuchukua kiambulisho cha Ujasiriamali ili nao waweze
kuchang pato la taifa.
Wajasiriamali
wadogo wanaoishi kwenye kambi ya uvuvi ya Sabasaba, Wachimbaji wadogo wa madini
wa Saza na wajasiriamali wegine Wilayani Songwe wamezipongeza juhudi za
serikali za kuweka mazingira mazuri ya ulipaji kodi kwa manufaa ya maendeleo ya
Taifa.
Simkonda
Maiko amesema anaipongeza serikali kwa kuwatambua wajasiriamali wadogo wadogo
na hivyo kuwawekea utaratibu mzuri wa kuchangia mapato pia itawasaidia kutosumbuliwa.
No comments:
Post a Comment