Spika
wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (kulia) akisalimiana na Waziri wa
Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani kabla ya kukagua miradi ya umeme Vijijini, kwa
Vijiji vya Ngonga na Kongwa Mashariki Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Spika
wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai (kushoto) akimsikiliza Waziri wa
Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani kabla ya kuzungumza na wananchi wa Kijiji cha
Ngonga Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Katika ziara ya Waziri Kalemani ya
kukagua miradi ya umeme Vijijini, kwa Vijiji vya Ngonga na Kongwa Mashariki
Spika
wa Bunge, Mhe. Job Ndugai akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Ngonga Wilayani
Kongwa Mkoani wa Dodoma.
Waziri
wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akizungumza na wananchi wa Kijiji cha
Ngonga (hawapo pichani) Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma. Kabla ya Kukagua miradi
ya umeme Vijijini, kwa Vijiji vya Ngonga na Kongwa Mashariki Wilayani Kongwa
Mkoani Dodoma. Wa pili kushoto waliokaa ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa,
Mhe. Job Ndugai. Akiwa kijijini hapo, Dkt. Kalemani aligawa kwa wananchi vifaa
20 vya umeme tayari (UMETA) ambapo wananchi hao wataunganishwa umeme bila
kuingia gharama ya kutandaza nyaya ndani ya nyumba.
Waziri
wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uwashaji wa umeme
katika Kijiji cha Kongwa Mashariki kilichopo Wilayani Kongwa Mkoani Dodoma.
Kulia kwake ni Spika wa Bunge na Mbunge wa Kongwa, Mhe. Job Ndugai. (PICHA NA DEONISIUS SIMBA OFISI YA BUNGE)
No comments:
Post a Comment