HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

April 04, 2019

Mambo 5 nyuma ya kifo cha Nipsey Hussle

Nipsey Hussle.
 
LOS ANGELES, MAREKANI

 KIFO kifo, ukitaka kujua ubaya wa kifo fika hospitalini, utakuta wengine wanalia, wengine hawana miguu tena, wengine wana vidonda, wengine wana vipele, wengine wana ukurutu, wengine wamezaa watoto wamekufa, kwa sababu yako wewe kifo.

Kifo kwa nini unatusumbua, tumezaliwa kwa sababu ya kuishi, ulimwengu bila watu si ulimwengu tena, kifo wee! Kifo wee kifo kifo hakina huruma.

Kifo we kifo tulikuwa tuna baba yetu, tulikuwa tunamtegemea, kifo umemchukua baba yetu, sasa tunakwenda tunahangaika hatuna mahala pa kulala.

Wakati baba alikuwa yupo watu walikuwa chungu tele, leo baba hayuko tena wengine wanatusimanga, wengine wanatuzunguka, sababu yako wewe kifo.

Haya ni sehemu ya maneno mazito yaliyo katika wimbo wa Kifo (Hakina Huruma) uliopata umaarufu mkubwa miaka ya 1980 ulioimbwa na nguli wa muziki wa dansi nchini Ramazani Mtoro Ongala ‘Dk. Remmy’.

Kifo kimemchukua rapa Ermias Joseph Asghe ‘Nipsey Hussle’ (33), aliyeuawa kwa kupigwa risasi nje ya duka lake la kuuza nguo jijini Los Angeles, nchini Marekani.

Nipsey Hussle, ambaye aliuawa kwa kupigwa risasi Jumatatu iliyopita, Aprili 1 mwaka huu, tukio hilo lililopelekea watu wawili kujeruhiwa.

Katika kisa hicho cha ufyatulianaji risasi kilichotokea nje ya duka la Marathon saa 1:00 asubuhi kwa saa za Marekani, liliacha simanzi kwa wadau wa burudani.


TETESI KUHUSU KIFO
Saa chache baada ya kifo cha Nipsey Hussle, mengi yamezungumzwa ikiwemo hili kubwa ambalo Serikali ya Marekani inahusishwa katika mauaji hayo.

Wengi wanaamini kwamba Nipsey ameuawa kutokana na harakati zake za kutaka kuachia kanda fupi (documentary), ambayo

inaelezea kwa kina tiba ya dawa ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) pamoja na Saratani, dawa ambayo iligunduliwa na Dk. Sebi.

Kuachiwa kwa kazi hiyo (documentary) na kuiweka wazi dawa ya VVU na Ukimwi kungepelekea serikali ya Marekani kukosa fedha ambazo tayari imekuwa ikiingiza kwa kutengeneza kinga pamoja na dawa za kupunguza makali.

Sasa Nipsey alikuwa akiweka wazi juhudi za kutaka kuachia kazi hiyo, na ndio inatajwa kuwa chanzo cha kifo chake.

Muigizaji na Muimbaji Nick Cannon kutoka nchini Marekani, ameibuka kupitia Instagram na kuandika kwamba ataendelea kuyaenzi ambayo Nipsey ameyaacha ikiwemo hili la kuiachia ‘documentary’ ya Dk. Sebi, na kusisitiza kuwa hawawezi kuwaua wote; “Can't Kill us ALL” na ataimailizia na kuiachia ‘documentary’ hiyo.


MAUZO YA ALBUM KUPANDA

Kifo cha rapa Nipsey Hussle kimepelekea kuongezeka kwa mauzo ya kazi zake kwenye mitandao mbalimbali ya kusikiliza na kupakua nyimbo duniani ikiwemo kwenye chati za iTunes na Amazon.

WASANII WENZAKE WAMLILIA

Wasanii maarufu nchini Marekani wakiwemo Drake, Rihanna na J Cole wametoa rambi rambi zao kufuatia kifo cha rapa huyo, Drake


alimuelezea marehemu kama; “Mtu maarufu mwenye heshima,” huku Rihanna akiandika katika mtandao wake wa Twitter: “Hii haingii akilini, nimeumizwa sana na tukio hili!,” aliandika Rihanna.

MTUHUMIWA ATIWA MBARONI
Eric Holder

Mtuhumiwa namba moja wa mauaji ya rapa Nipsey Hussle, Eric Holder amewekwa kwenye jela ya pekee yake baada ya kukamatwa juzi asubuhi.

Polisi wa Los Angeles wameeleza kwamba kutomchanganya mtuhumiwa huyo na watu wengine ni kwa sababu za usalama wa maisha yake.

Eric ataendelea kubaki humo hadi tarehe ya kusikilizwa kwa kesi yake itakapotajwa.


Dhamana imetajwa pia, ni Dola za Kimarekani Milioni 7 ambazo ni sawa na Sh. Bilioni 16 ambazo inaaminika hatoweza kumudu mzigo huo.


UJUMBE WAKE WA MWISHO KABLA YA KIFO

Nipsey Hussle; “Having strong enemies is a blessing.” aliandika kwenye ukurasa wake wa twitter, akimaanisha kuwa; “Kuwa na maadui wenye nguvu ni Baraka.”


Makala hii imeandaliwa na Yassin Lupatu kwa msaada wa mitandao mbalimbali ya kijamii.

No comments:

Post a Comment

Pages