NA JOHN MARWA
LICHA ya kuwachapa Azam FC Kocha Mkuu wa Yanga SC ameweka
wazi kuwa hawako kwenye mawazo ya ubingwa kwa sasa kutokana na michezo
waliosalia nayo kulinganisha na mpinzani wao Simba SC.
Ushindi huo wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC umewafanya
vinara hao wa Ligi Kuu Tanzania Bara TPL kufikisha pointi 77 za michezo 33,
wakiwaacha wapinzani wao kwa pointi nane huku kabla ya mtanange wao wa jana
dhidi ya JKT Tanzania.
Yanga wamesaliwa na mechi tano mkonono kukalisha duru
ya TPL msimu huu huku watani zao wakiwa na michezo 11 wakizidiana pointi nane pekee.
Kama simba wanashinda michezo mitatu iliyombele yao
watapita Yanga kwa pointi moja huku wakisaliwa na michezo nane kuhitimisha TPL
2018/19.
Katika mtange huo wa juzi uliopigwa Dimba la Uhuru
jijini Dar es Salaam ulikuwa wa kimbinu zaidi kwa vinara hao ambazo ziliwafanya
kuondoka na pointi tatu mujarabu kwa bao la mkongwe Anko Mrisho Ngasa akimalizia
krosi ya Ibrahim Ajibu kutoka kaskazini mashariki mwa uwanja.
Baada ya pambano hilo kumalizika Zahera alisema kwa
sasa hatima ya ubingwa haiku mikononi mwao kutokana na tofauti ya michezo
waliyonayo na wapinzanbi wao Simba.
Lakini pia alisema Simba wamekuwa wakitengenezewa
mazingira ya kutetea taji hilo huku wao wakifanyiwa fitna kwenye baadhi ya
michezo yao.
!! kwa sasa siwezi kusema chochote kuhusu ubingwa,
hauko mikononi mwetu, kama Ligi ingekuwa inasimamiwa kama zile za Ulaya basi
nadhani tungekuwa tumeshatwaa ubingwa tayari.
!!Tumebakiwa na michezo mitano lakini mpinzani wetu
ana michezo zaidi ya 10 na tofauti ya pointi ni tano, hapo siwezi kusema kuwa
tunaweza kutwaa ubingwa. Haukuko mikononi mwetu tena kwa namna Ligi
inavyoendeshwa.!!alisema Zahera na kuongeza kuwa.
!!Kumekuwa na vitendo vingi vinavyoshusha hadhi ya
Mpira wetu kama juzi kule mwanza kilichotokea kwenye mchezo wa KMC dhidi ya
Simba ni aibu, hauwezi kuwa bingwa kwa naman ile.
!!Niwapongeze TFF kwa kuchukua hatua kwa waamuzi
waliochezesha ule mchezo nadhani wanapaswa kufanya vile kila inapotokea ili
mpira wetu uweze kupiga hatau.alisema zahera.
No comments:
Post a Comment