Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk Hamisi Kigwangalla (watatu kulia)
akizindua mbio za kilometa 21 za Ngorongoro Race 2019 katika lango kuu
la kuingilia na kutokea Hifadhi ya Ngorongoro zilizofanyika Aprili 20, 2019. Kigwangalla mbali na
kuzindua mbio hizo pia alishiriki na kumaliza kilometa 21. (Na
Mpiga Picha Wetu).
NA MWANDISHI WETU, KARATU
WANARIADHA wa Tanzania, walishindwa kutamba
mbele yak Wakenya katika mashindano ya Mbio za Ngorongoro (Ngorongoro Race
2019), baada yakushika nafasi za pili katika mbio za Kilomita 21.
Katika mbio hizo zilizoanzishwa na Waziri wa
Maliasili na Utalii Dk. Hamis Kigwangalla, kwenye lango kuingilia Mamlaka yak
Hifadhi yak Ngorongoro (NCAA), nakumalizikia viwanja vya Mazingira Bora mjini
Karatu, ilishuhudiwa Esther Chesang akishinda baada ya kutumia saa 1:16.41 kwa
upande wa wanawake.
Wakati Chesang akiibuka kinara wa wanawake, Abraham
Too alishinda kwa upande wa wanaume, akikimbia kwa saa 1:05.39, akifuatiwa na
Michael Kishiba ‘Msukuma’ wa JKT aliyetumia saa 1:05:45, akifuatiwa na Festus
Cheboi 1:05.47 wa Kenya.
Kwa upande wa wanawake, Watanzania Natalia Elisante
kutoka klabu ya Talent jijini Arusha alimfuatia Chesang akitumia 1:16:49, huku
nafasi ya tatu ikienda kwa Angelina Tsere wa JKT aliyetumia saa 1:18.57.
Kwenye mbio za Kilomita wanawake, Cecilia Pangawa
JWTZ alishinda akitumia dakika 16:37.29 akifuatiwa na Sarah Hiitiwa JKT dakika
17:08.66 huku nafasi ya tatu ikienda kwa Sara Ramadhani wa Arusha dakika 17:13.36.
Kwa upande wa wanaume Kilomita 5, mshindi wa kwanza
alikuwa Ambroce Sadikiel wa Tanzania aliyetumia dakika 14:14.56, huku Marco
Sylvester wa JKT alimaliza wa pili akitumia dakika 14:23.09 wakati mshindi wa
tatu ni Daniel Sinda aliyetumia dakika 14:26.47.
Mshindi wa kwanza kwa wanawake na wanaume katika
Kilometa 21 aliondoka na kitita cha Sh. Mil. 1 huku wapili akitwaa Sh. 500,000
na watatu Sh. 300,000.
Akizungumza baada ya kuibuka mshindi, Chesang
alisema mbio zilikuwa ngumu, kwani wanariadha wengi walikuwa wamejiandaa ila
yeye kujituma zaidi ndio ilikuwa siri ya mafanikio.
Kwa upande wake, Natalia alisema anamshukuru Mungu
kwa nafasi aliyoipata ya pili, lakini si kwamba Watanzania hawawezi bali
inahitajika sapoti zaidi hususan kwa wanariadha wa kike wanaochipukia.
Kwa mara ya pili mfululizo, mgeni rasmi Dk.
Kigwangalla, mbali ya kuwa mgeni rasmi alishiriki kikamilifu mbio za Kilomita
21 na kumaliza.
Mbali na Dk. Kigwangalla, viongozi mbalimbali akiwemo
Mhifadhi Mkuu wa NCAA, Dk. Fred Manongi, Wabunge Wajumbe wa Kamati ya Bunge ya
Ardhi, Maliasili na Utalii walishiriki lakini wengi wao hawakuweza kumaliza
Kilomita 21.
Akizungumza baada ya mbio hizo, Dk. Kigwangalla
alisema kuwa mbio kama hizo zina faida nyingi ikiwemo kuweka sawa afya pamoja
na kuondoa msongo wa mawazo na pia kiuchumi Karatu imefaidika kwa watu kulala,
na kununua vitu mjini hapo, hivyo wameongeza pato.
Alisema ni aibu kubwa na inauma sana kutoa zawadi
kwa Wakenya, kwani alitaka fedha hizo zingechukuliwa na Watanzania.
Aidha, Dk. Kigwangalla, alisema atamuomba Waziri
Mkuu kuitisha kikao cha mawaziri kadhaa ili kuona wataandaa vipi timu ya taifa
ya riadha na sio kuwaachia RT pekee yao ili kuhakikisha Tanzania inafanya
vizuri katika mashindano yak kimataifa.
Pia, alisema NCAA katika bajeti yao safari hii
imetenga bajeti kidogo kuanza utekelezaji wa agizo lake la mwaka jana kutaka
ijengwe Academy ili kuibua na kuendeleza vipaji vya vijana katika mchezo wa
riadha.
No comments:
Post a Comment