HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 01, 2019

BENKI YA CRDB YAKUTANA NA WAWEKEZAJI WAKE DAR




Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akisalimiana na baadhi ya wawekezaji wa benki hiyo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akibadilishana mawazo na baadhi ya wawekezaji wa benki hiyo.

Sehemu ya watu waliohudhulia mkutano huo.

Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, akizungumza katika mkutano na wawekezaji wa benki hiyo.

Naibu Gavana wa Benki Kuu, Dk. Bernard Kibesse (kulia) akifurahia jambo na Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati).
Mkurugenzi wa Masoko, Utafiti na Huduma kwa Wateja, Tully Mwambapa, akimkaribisha Mkurugenzi Mtendaji wa benki hiyo, Abdulmajid Nsekela. 

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na wawekezaji wa benki ya CRDB.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akizungumza na wawekezaji wa Benki ya CRDB juu ya maendeleo ya benki hiyo jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay (kulia), akimpongeza Mkurigenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela baada ya kutoa mada.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo, akitoa taarifa za fedha.
Mkurugenzi wa Fedha wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo, akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Bodi, Ally Laay.

Naibu Gavana wa Benki Kuu (BoT), Dk. Bernard Kibesse (kushoto), akiwa na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB, Ally Laay, wakati wa hafla iliyoandaliwa na Benki ya CRDB kwa ajili ya Wawekezaji wake.

Mgeni rasmi Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bernard Kibesse, akizungumza na wawekezaji wa Benki ya CRDB.
 Katibu wa Benki ya CRDB, John Rugambwa, akimpongeza mgeni rasmi Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Bernard Kibesse, baada ya hotuba ya ufunguzi.
Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya CRDB akisoma taarifa mbalimbali zinazohusu benki hiyo.

Mkurugenzi wa Fedha Benki wa Benki ya CRDB, Fredrick Nshekanabo, akipitia jarida la benki hiyo.
Kutoka kulia ni Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela na Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya CRDB, Ally Laay.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela (katikati), akisalimiana na Naibu Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Dk. Bernard Kibesse, wakati wa mkutano na wawekezaji wa CRDB juu ya maendeleo ya benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam juzi. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Benki hiyo, Ally Laay.

Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, akibadilishana mawazo na Mkurugenzi Mtendaji wa Mwananchi Communications, Francis Nanai.

Baadhi ya wawekezaji wa Benki ya CRDB wakiwa katika mkutano huo.

Baadhi ya wakurugenzi wa Benki ya CRDB.


Picha ya pamoja.




Na Mwandishi Wetu

SERIKALI imesema mazingira wezeshi yaliyowekwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT), yameifanya Benki ya CRDB kuwa benki kubwa hapa nchini inayochagiza uchumi hasa kwenye miradi mikubwa ya serikali.

Akizungumza jijini Dar es Salaam Aprili 30, 2019 wakati uongozi wa CRDB ulipokutana na wawekezaji wake, Naibu Gavana wa BoT, Dk. Bernard Kibesse, alisema mazingira wezeshi yamewekwa kwaajili ya benki zote hapa nchini hivyo ni muda wao kuyatumia ili kukua kama ilivyofanya CRDB.

Aliyataja mazingira wezeshi kuwa ni kudhibiti mfumuko wa bei usiozidi asilimia nane huku akisisitiza kwamba sera nzuri za uchumi zimeufanya uchumi wa nchi hii kukua kwa asilimia saba kwa miongo mitatu mfululizo.

"Mmeona ukuaji wa CRDB wana mali za matrilioni ya shilingi wana mtandao mkubwa wa matawi kote nchini na kikubwa wameshusha riba za mikopo yao," alisema Dk. Kibesse.

Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Abdulmajid Nsekela alisema mafanikio ya benki hiyo kwenye robo ya kwanza ya mwaka 2019 ni matokeo chanya ya utendaji wa watumishi, wateja na wawekezaji wa benki hiyo kubwa hapa nchini.

"Kwenye robo ya kwanza namba zinasoma vizuri maana tumeiona faida ya Sh. Bilioni 30.7 hiyo ni karibu nusu ya faida ya benki mwaka jana yaani 2018.

"Tumeongeza namba ya wateja hadi kufikia zaidi ya milioni tatu, matawi yetu yapo 265 nchi nzima, ATM 550 na mawakala milioni nane kote Tanzania kwa hiyo maanikio haya yataendelea ndio maana tunasema CRDB ni benki kubwa hapa nchini," alisema Nsekela.

Alisema ukuaji wa benki hiyo umechagizwa na ushiriki wao kwenye miradi mikubwa ya serikali ukiwema wa treni ya kasi na umeme wa Mto Ufiji (stigullers gage).

Kwa mujibu wa Nsekela, mwaka 2018 CRDB imetoa mikopo ya Sh.trilioni 3.2 kwa wakulima na wafanyabiashara wa kada zote hapa nchi na kubainisha kuwa kiwango hicho kitaongezeka mwaka huu.

No comments:

Post a Comment

Pages