HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

May 01, 2019

WAFANYAKAZI SHIRIKA LA POSTA WALIVYOSHIRIKI MEI MOSI 2019

Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda, akiwahutubia wafanyakazi katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam leo.
Mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mhe. Paul Makonda (wa pili kushoto), akiwa pamoja na Wakuu wa Wilaya (kulia) na viongozi wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi nchini (TUCTA), wakiimba wimbo wa mshikamano, katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam leo.
 Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakisakata rumba katika gari lao la matangazo kabla ya kuingia katika viwanja vya uhuru kwa ajili ya maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani (Mei Mosi), jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakiwa nje ya uwanja wa Uhuru tayari kuingia uwanjani kwa maandamano katika maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi Duniani.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakiwa wamebeba bango lenye ujumbe wa maadhimisho ya Siku ya Wafanyakazi, ndani ya Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta wakiwa wenye furaha huku wamebeba bango lenye ujumbe maalum wakipita mbele ya mgeni rasmi,Jijini Dar es salaam.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakipita mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda, na bango lao lenye ujumbe maalum.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakimpungia mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, wakati wakipita na bango lao.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakiwa na furaha huku wamebeba miavuli yao, wakipita kwa maandamano mbele ya mgeni rasmi, Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), wakifurahi wakiwa kwenye jukwaa kumsikiliza mgeni rasmi Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda.
Wafanyakazi wa Shirika la Posta Tanzania wakipita na Pikipiki zao za kutolea huduma mbalimbali za Shirika mbele ya mgeni Rasmi.
Magari ya kusafirisha vifurushi na kutoa huduma zingine za Shirika la Posta Tanzania yakipita kwa msafara mbele ya mgeni katika viwanja vya Uhuru, jijini Dar es Salaam. 
Meneja Rasilimali watu, Miriam Mbaga kwa niaba ya Postamasta Mkuu, akimkabidhi cheti mfanyakazi hodari kitaifa wa Shirika la Posta, Madaraka Simba (kulia), katika maadhimisho ya Mei Mosi, mkoani Mbeya.
Meneja Rasilimali watu, Miriam Mbaga kwa niaba ya Postamasta Mkuu, akimkabidhi cheti mfanyakazi hodari wa Mkoa wa Mbeya, Godwin Davis (kulia), katika maadhimisho ya Mei Dei, mkoani humo.
Mwenyekiti (TEWUTA) Makao Makuu Shirika la Posta, Aneth Mdamu, katika hafla fupi ya kumpongeza mfanyakazi bora kitaifa wa Shirika la Posta, Madaraka Simba.
Meneja wa Shirika la Posta mkoani Mbeya, Abdon Mahimbo (katikati mwenye koti), akiwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi walioshiriki sherehe za Mei Mosi, jijini humo.

No comments:

Post a Comment

Pages