HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 19, 2019

AIRTEL YAONGEZA VIFAA ZAIDI YA 4,000 USAJILI WA ALAMA ZA VIDOLE

Meneja uhusiano wa Airtel Tanzania bw, Jackson Mmbando akionesha baadhi ya vifaa vipya kati ya 4,000 vilivyotolewa na Airtel kwaajili ya usajili wa alama za vidole. Airtel inaendelea na usajili huo na imeongeza vifaa Zaidi ya 4,000 ili kukamilisha zoezi hilo kama ilivyoagizwa na mamlaka ya mawasiliano (TCRA) kuwa kila mteja wake awe amesajiliwa hadi kufikia desemba mwaka huu. Meneja Uhusiano wa Airtel, Jackson Mmbando na Meneja usajili wa Airtel bi Angestina Mahatane wakionesha kati ya 4,000 vifaa vipya vilivyonunuliwa na Airtel ili kutumika katika usajili mpya wa teknolojia ya  mfumo wa alama za vidole. Airtel imetangaza kuongeza vifaa hivyo ili kutimiza agizo lilitolewa na mamlaka ya mawasiliano TCRA kuwa hadi desemba 31 wateja wote wa Airtel wawe wamesajiliwa upya kwa kutumia mfumo huo wa kisasa unaohusisha alama za vidole. 


Na Mwandishi Wetu

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel inayomilikiwa na Bharti Airtel pamoja na serikali ya jamuhuri ya muungano Tanzania imesaambaza vifaa vipya zaidi 4,000 kwaajili ya usajili unaotumia alama za vidole nchini huku wakiendea na usajili huo katika wiki ya utumishi wa umma inayoendelea kati ya 17 hadi 21 Juni huku.

Akielezea mikakati yao ya kusajili wateja wake nchini Meneja mawasiliano wa Airtel Tanzania Jackson Mmbando alisema “ vifaa zaidi ya 4,000 vimesambazwa katika maduka ya Airtel pamoja na taasisi mbalimbali za huduma kwa jamii ili kuendelea kuhudumia wateja wanapokwenda kusajili upya laini zao kwa kutumia alama za vidole”

Mmbando alitoa wito kwa wateja kuzingatia usajili huo muhimu kama ilivyoagizwa na mamlaka ya mawasiliano nchini (TCRA) ili kuepuka kuja kufungiwa laini zao ifikapo Desemba.

“Pia Tumeshapanga kushirikiana na uongozi wa taasisi binafsi na zile za serikali zaidi ya 40 ndani mwezi huu na mwezi Agosti ili kuendelea kuwasajili wafanyakazi na watumishi katika maeneo yao ya kazi bila wao kuja katika maduka yetu” alileza Mmbando

Taasisi tunazopanga kuzitembelea saa ni pamoja na Arusha Technical College (ATC), Eastern and Southern African Management Institute (ESAMI), Institute of Accountancy Arusha (IAA), Tumaini University Makumira (TUMA), University of Arusha (UoA).

zingine ni Institute of Finance Management (IFM) (Mwanza, Catholic University of Health and Allied Sciences (CUHAS), College of Business Education (CBE) Mwanza, Institute of Rural Development Planning (IRDP),Mwanza,St. Augustine University of Tanzania (SAUT), Tanzania Institute of Accountancy (TIA), Mwanza.

Kwa mkoa wa morogoro ni Muslim University of Morogoro (MUM), Sokoine University of Agriculture (SUA), Mzumbe University (MU).

Mkoa wa Mbeya na Iringa tutatembelea Mbeya University of Science and Technology (MUST), Mzumbe University –Mbeya University College (MUMCo), Tanzania Institute of Accountancy (TIA),Mbeya, Mkwawa University College of Education (MUCE), University of Iringa(UoI).

Zoezi la usajili kwa kutumia alama za vidole lilianza rasmi Mei 1 mwaka huu baada ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) kuzindua mfumo huo na kisha kutoa mwongozo kwa makampuni yote ya simu kufanya usajili wa laini za simu upya kwa kutumia alama za vidole hadi Desemba mwaka huu kila mteja wake awe amesajiliwa.

No comments:

Post a Comment

Pages