HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 06, 2019

KALA JEREMIAH AREJEA KWA KISHINDO NA VIDEO MBILI KWA MPIGO



Dar es Salaam, Tanzania

BAADA ya ukimya wa zaidi ya mwaka mmoja, mkali wa Muziki wa Hip Hop nchini, Kala Jeremiah, ameachia kibao kipya kinachoitwa Nisamehe, ambacho Ijumaa hii ya Juni 7 anaachia video yake na nyingine ya Amerika, kupitia utambulisho alioupa jina la Double Release.

Kala Jeremiah, aliyetikisa na vibao kadhaa vikiwemo Dear God, Kijana, Usikate Tamaa, Wana Ndoto na nyinginezo, amewataka mashabiki kuhakikisha hawapitwi na burudani kali sambamba na ujumbe mzito unaopatikana katika vibao vyake hivyo.

Akizungumza na HABARI MSETO, Kala Jeremiah alizitaja video anazoachia Ijumaa hii na ambazo zitapatikana kwenye Chanel yake ya You Tube kuwa ‘Nisamehe’ aliomshirikisha Aslay na Amerika alichofanya na msanii anayetambulika kwa jina la Zest.

“Kwa sasa nawaalika mashabiki zangu kusikiliza audio ya kibao kipya kiitwacho Nisamehe, ambacho Ijumaa ya Juni 7 nitatambulisha video ya kibao hicho nilichomshirikisha Aslay, pia utambulisho huu nilioupa jina la Double Release utabeba video  ya wimbo Amerika niliofanya na Zest,” amesema Kala Jeremiah.

No comments:

Post a Comment

Pages