HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 25, 2019

KAMPUNI YA CANDY & CANDY YAWAKUMBUKA YATIMA ARUSHA

 Mkurugenzi wa Kampuni ya Candy &Candy, Joe Kariuki (mwenye kofia), akigawa juisi na biskuti kwa watoto yatima kwenye kituo cha Faraja cha jijini Arusha akiwa na watendaji wengine wa kampuni yake.
 Mkurungenzi wa Kampuni ya Candy & Candy Joe Kariuki akimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Faraja, Faraja Mollel, ndoo ya mafuta ikiwa ni sehemu ya vyakula walivyopeleka kituoni hapo mwanzoni mwa wiki.
 Mkurungenzi wa Kampuni ya Candy & Candy Joe Kariuki akimkabidhi Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Faraja, Faraja Mollel, ndoo ya mafuta ikiwa ni sehemu ya vyakula walivyopeleka kituoni hapo mwanzoni mwa wiki.
Mkurugenzi wa Kituo cha Watoto Yatima cha Faraja, Faraja Mollel (kushoto), akitoa maelezo ya kituo hicho kwa mkurugenzi wa kampuni ya Candy &Candy, Joe Kariuki (mwenye kofia), mwanasheria wa kampuni hiyo, Lilian Joel na Rais wa programu ya vijana ya U and I inayoendeshwa  na kampuni hiyo, Nasra Swai wakati walipotembelea kituo hicho mwanzoni mwa wiki.


NA MWANDISHI WETU, ARUSHA

KAMPUNI ya Candy & Candy imetoa misaada wa vyakula, vinywaji baridi na fedha za kununulia nguo za ndani watoto yatima wanaolelewa kwenye kituo cha Faraja cha jijini Arusha.

Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joe Kariuki juzi aliongoza wafanyakazi wa kampuni hiyo kugawa vitu hivyo pamoja na kuongea na watoto wa kituo hicho zaidi ya 200.

Alisema kuwa kampuni ya Candy & Candy itaendelea kuwa karibu na kituo hicho ambapo aliahidi kurudi kituoni hapo baada ya miezi miwili na endapo akiwakuta wamebadilika na kuwa na mwenendo mwema basi atawapatia zawadi ya luninga.

"Baba yenu (Faraja) ameniambia hapa kuna waliokuwa wamehukumiwa na kufungwa, tunashukuru sasa mko kwenye hiki kituo mnalelewa vizuri basi badilikeni tabia ili msirudi tena kule kwenye matatizo," alisema
Kariuki na kuongeza.

"Nitakuja hapa baada ya miezi miwili, baba yenu akiniambia
mmebadilika tabia, hampigi watoto wa majirani na mnafanya usafi wa mwili (kuoga) nitawanunulia TV nitaifunga hapo (akionyesha ukutani),".

Mkurugenzi huyo wa Candy& Candy ambaye kampuni hiyo ina matawi nchi mbalimbali huku makao makuu yake yakiwa nchini ,Uingereza alitoa fedha kwa ajili ya kusaidia masomo ya ziada ya mwanafunzi, Barakaeli ambaye alidai kuwa endapo asingelipa kwa siku ya jumatatu basi asingeruhusiwa
kuingia darasani kujifunza.

Aidha walikabidhi kituoni hapo kilo 100 za mchele, unga wa mahindi gunia nne, mafuta ya kupikia ndoo mbili zenye lita 20 pamoja na juisi na biskuti ambazo waliwagawia watoto kituoni hapo.

Kariuki alilazimika kutoa fedha kwa ajili ya kuwanunulia nguo za ndani watoto wenye umri wa kati ya miaka tisa na 16 kwenye kituo hicho baada ya kumweleza kuwa wengi wanayo moja huku wachache wakiwa na ambazo hazizidi tano.

Naye Rais wa programu ya U & I, (you and I) inayoendeshwa na Candy & Candy, Nasra Swai akiongea na watoto wenye umri wa kati ya miaka tisa na 17 aliwaleza umuhimu wa kujitambua kama watoto.

Aidha ali waeleza watoto hao jamii inawapenda na kuwathamini ndiyo sababu wamefika kwenye kituo hicho kuongea nao na kubadilishana mawazo ambapo aliwaahidi kurudi tena kwenye kituo hicho kwa ajili ya kuzungumza nao juu ya masuala mbalimbali ya makuzi.

Akiongea kwa niaba ya watoto kwa niaba ya wenzake mtoto, Barakaeli Faraja alisema kuwa wanashukuru kampuni hiyo kuwasaidia kupata vitu hivyo kwani wmekuwa wakivihitaji kwa muda mrefu.

Aliiomba kampuni hiyo iangalie uwezekano kuwasaidia zaidi kuwalipia ada baadhi ya watoto, kupata vitanda kwani kwa sasa wanabanana mno, kompyuta na runinga kwa ajili ya chumba cha watoto wakubwa.

Mkurugenzi wa kituo hicho, Faraja Mollel alisema kuwa wanakabiliwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa chakula cha kutosha kwa ajili ya watoto hao ambapo wakati mwingine huwapa milo miwili tu kwa siku.

Alisema kuwa yeye aliguswa kuanzisha kituo hicho kutokana na historia ya maisha yake ambapo yeye akiwa na umri mdogo aliwahi kuishi kwenye mitaa ya jiji la Arusha akiwa na dd yake, Jenipher ambaye kwa sasa anaishi Marekani.

Alisema kuwa walipata msamaria mwema mama wa Kizungu ambaye aliwachukua na kwenda kuishi nao ndipo maisha yao yalipobadilika hivyo baada ya kufanikiwa akaguswa kuwasaidia watoto waliopitia magumu kama ya kwake.

Faraja alisema kuwa awali kwenye kituo hicho hapakuwa na shida ya ada kwa watoto a kituo hicho kwani kulikuwa na mfadhili ambaye alikuwa akiwasaidia kununua chakula na kulipia ada baadhi ya watoto hao lakini alifariki mwaka jana jambo linalowaweka katika wakati mgumu kwa sasa.

No comments:

Post a Comment

Pages