HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2019

MABONDE YA MAJI KUFANYIWA UTAFITI

 KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo wakati alipotembelea mradi wa Kunusuru vyanzo vya maji na Matumizi Bora ya Ardhi (Securing Watershed through Sustainable Land Management) wilayani Muheza unaotekelezwa na Bonde la Maji la Pangani pamoja na Bonde la Wami Ruvu kwa kushirikiana na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga, Dar es Salaam na Morogoro (Tanga UWASA, DAWASA na MORUWASA.
 KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kushoto akitazama mpaka wa bwawa la maji la Mabayani Jijini Tanga wakati wa ziara yake mkoani Tanga kulia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly
  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kushoto akitoka kutazama  mpaka wa bwawa la maji la Mabayani Jijini Tanga wakati wa ziara yake mkoani Tanga
  KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kushoto akimsikiliza kwa umakini Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Goefrey Hilly kulia aliyevaa koti  wakati wa ziara yake.
 AFISA Uhusiano wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga ( Tanga Uwasa) Dorrah Kilo kushoto akimuelezea jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo wakati wa ziara yake ya siku moja Jijini Tanga na wilayani Muheza.
 Muonekano wa eneo la kutirirsha maji eneo la bwawa la Mabayani Jijini Tanga mara baada ya Maji kujaa bwawani kama linavyoonekana wakati wa ziara hiyo.
 Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kushoto akimtua mama ndoo wakati wa ziara yake akiwa kwenye eneo la Mashewa wilayani Muheza mara baada ya kutembelea mradi ya upandaji wa vitalu vya miti ya mitikiti.
 Mwenyekiti wa Kikundi cha Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kulia akimuonyesha Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo namna wanavyopanda miti ya mitikiki wanaoshuhudia wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly.
  Mwenyekiti wa Kikundi cha Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akiwa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji katikati Proffesa Kitila Mkumbo na Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara hiyo.
  Mwenyekiti wa Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akimkabidhi zawadi Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Safi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga Uwasa) Mhandisi Geofrey Hilly wakati wa ziara ya Katibu Mkuu wa wilaya ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo anayeshuhudia katikati.
Mwenyekiti wa Uwamakizi wilayani Muheza Twaha Rajabu kushoto akimkabidhi zawadi Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo kulia anayeshuhudia ni Mkurugenzi wa Tanga Uwasa Mhandisi Geofrey Hilly.


Na Mwandishi Wetu

KATIBU Mkuu wa Wizara ya Maji Proffesa Kitila Mkumbo ameagiza mabonde yote tisa ya Maji nchini kuhakikisha wanafanya utafiti ili kuweza kutambua mazao rafiki ambayo wananchi wanaweza kulima bila kuathiri vyanzo vya maji vilivyopo ili viendelee kuwa endelevu.

Proffesa Mkumbo aliyasema hayo leo wakati alipotembelea mradi wa Kunusuru vyanzo vya maji na Matumizi Bora ya Ardhi  (Securing Watershed through Sustainable Land Management)  unaotekelezwa na Bonde la Maji la Pangani pamoja na Bonde la Wami Ruvu kwa kushirikiana na Mamlaka za Majisafi na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga, Dar es Salaam na Morogoro (Tanga UWASA, DAWASA na MORUWASA)

 Pia Katibu huyo alitembelea Umoja wa Wakulima wa Hifadhi Mazingira Kihuwi Zigi (UWAMAKIZI) huku akionyeshwa kuridhishwa na namna wanavyotunza vyanzo vya maji kwenye maeneo yao jambo ambalo alisema linapaswa kuigwa mfano na maeneo mengine hapa nchini.

 Alisema katika jambo hilo wananchi wanapaswa kutambua mazao ambayo wanaweza kulima kwenye maeneo hayo ambayo yatakuwa tija kwao kuwakomboa kiuchumi bila kuleta athari za uharibifu wa vyanzo vya maji vilivyopo ili viendelee kuwepo kwa manufaa vya vizazi vya sasa na vijavyo.

 "Mazao ni mengi mnaweza kulima kwenye maeneo mengine hivyo lakini ni muhimu kwamba mhakikishe mnafanya utafiti kuweza kubaini ni mazao gani mnaweza kulima bila kuathiri vyanzo vya maji "Alisema

Aidha alisema baada ya kutembelea na kuona mafanikio yaliyopo amesema amejifunza kwamba mradi ambao wananchi wakishirikishwa na kushiriki ikiwemo kuelimishwa wanakuwa msaada mkubwa kwenye kutunza vyanzo vya maji kama alivyoona kwenye Mito hiyo aliyotembelea maji ni mazuri kabisa.

Katibu huyo alisema pia utunzaji mzuri wa maji hayo umesaidia kulinda bwawa la Mabayani na kupelekea gharama za kusafisha maji kupungua huku wananchi wakishirikishwa kutunza bwawa hilo kupitia mradi huo ambao pia umesaidia kuweka mipaka  kati ya bwawa na walipo wananchi.

Hata hivyo alieleza kwamba katika maeneo hayo mradi unapotekelezwa Mto Zingi na Ruvu wananchi wameelimishwa kulima mazao ambayo ni rafiki kwa mto ambayo hayana athari  hivyo Agizo la Rais Dkt John Magufuli la kutaka wananchji wasiondolee kwenye mita sitini ila waelimishwe limetekelezwa kwa asilimia kubwa  Tanga kupitia Tanga Uwasa na hivyo hakuna ugomvi.

No comments:

Post a Comment

Pages