HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 21, 2019

MASHINDANO YA KUUNDA TIMU YA WILAYA YAHITIMISHWA


Na Stephano Mango, Namtumbo

MASHINDANO ya UMISHUMTA kuunda timu ya wilaya ya Namtumbo yamehitimishwa jana katika viwanja vya shule ya msingi Namtumbo kwa washindi wa kwanza kupata ngao na kupatikana kwa wachezaji 75 kuwakilisha wilaya katika mashindano ya kimkoa

Mashindano hayo yamefanyika kwa muda wa siku mbili kukiwa na washiriki wapatao wanafunzi 234 na kati ya hao wasichana 123 na wavulana 111 kutoka katika klasta 5 kati ya 6 zilizopo katika wilaya ya Namtumbo.

Akiongea na wanafunzi mara baada ya kumalizika kwa mashindano hayo Ofisa elimu shule za Msingi Protas komba alisema kuwa amefurahishwa na wanafunzi kujituma katika michezo na kuwataka kuendelea kujituma .

Aidha komba aliwaagiza walimu wa michezo mashuleni kuhakikisha vipindi vya michezo vilivyowekwa katika ratiba zinafuatwa ili kuwapata wachezaji wenye viwango na wenye kujituma katika michezo hiyo.

Hata hivyo komba aliwataka wachezaji waliochaguliwa kuiwakilisha wilaya hiyo kwa kuonesha moyo wa uzalendo kwa wilaya yao kwa kujitoa kwa hali na mali kucheza kwa lengo la kuiwakilisha wilaya yao vyema.

Pamoja na hayo komba aliwataka wanafunzi wasiochaguliwa kuiwakilisha wilaya kutokata tamaa kwani alitamani kuwapeleka wote kutokana na viwango walivyoonesha lakini akadai nafasi zinazotakiwa ni chache .

Kwa upande wake Afisa michezo wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo John Ligoho awali alimweleza Afisa elimu wilaya kuwa mashindano yaliyofanyika yalikuwa ya mpira wa miguu kwa wavulana,mpira wa pete kwa wasichana ,mpira wa mikono,riadha kwa wasichana na wavulana pamoja na sanaa.

Mashindano hayo yalihitimishwa kwa washindi wa kwanza kupata ngao na kupatikana kwa wachezaji 75 wa kuiwakilisha wilaya ya Namtumbo katika mashindano hayo katika ngazi ya mkoa wa Ruvuma yatakayofanyika manispaa ya Songea.

No comments:

Post a Comment

Pages