Na
Frank Mvungi - MAELEZO
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) imetajwa
kuongeza tija katika utendaji wake kutokana na matumizi ya Teknolojia ya Habari
na Mawasiliano (TEHAMA)katika huduma zake kwa wadau.
Akizungumza katika kipindi cha “TUNATEKELEZA” Mkurugenzi Mkuu wa Tume hiyo Prof. Lazaro
Busagali amesema kuwa Tume hiyo imeimarisha utoaji wa huduma zake kwa wadau
kuanzia katika utoaji wa vibali na huduma zote ikiwemo za maabara.
“ Tunaipongeza na kuishukuru Serikali kwa
kuiwezesha Tume kuwa na Ofisi za Kanda
21 na asilimia 90 ya vibali vinatolewa ndani ya siku moja kutokana na
kuimarishwa kwa miundombinu yetu ya kutolea huduma “ Alisisitiza Prof. Busagali
Akifafanua Prof. Busagali amesema kuwa Teknolojia
ya nyuklia ikitumika vizuri inaleta matokeo chanya katika jamii kwa kuwa ni
muhimu katika kuchangia maendeleo kutokana na umuhimu wake katika kuchochea
maendeleo.
Akizungumzia utendaji wa Tume hiyo Prof. Busagali
amesema kuwa moja ya majukumu ya Tume ni kuhakikisha kuwa Taasisi zote
zinazotumia mionzi katika kutoa huduma zake zikiwemo Hospitali zinazingatia
matumizi bora ya mionzi kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu
zinazosimamia sekta hiyo.
Aliongeza kuwa Tume hiyo imekuwa ikifanya ukaguzi
wa mara kwa mara katika Taasisi zote zinazotumia mionzi hapa
nchini ili kuhakikisha kuwa watumiaji wa huduma za Taasisi husika wako salama
dhidi ya madhara yanayoweza kusababishwa na mionzi.
Aidha alifafanua kuwa, Tume imejiwekea utaratibu
wa kutoa elimu kwa wananchi na wadau ili
kuepuka matumizi ya mionzi yasiyozingatia sheria, kanuni na taratibu ili
kuepusha madhara ya mionzi hiyo pale inapotumika vibaya.
“Serikali ya Awamu ya Tano imetuwezesha kuwa na
maabara ya kisasa na pia wadau wetu ambao ni
Shirika la Nguvu za Atomiki Duniani kwa kutuwezesha kupata vifaa vya
kisasa vya maabara yetu” Alisisitiza Prof. Busagali.
Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania ni Taasisi ya
Serikali inayosomamia na kuratibu masuala yote yanayohusu mionzi hapa nchini
ikiwa na maabara ya kisasa ambayo ni mwanachama wa Shirika la Afya Duniani
(WHO).
No comments:
Post a Comment