HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 26, 2019

RAIS MAGUFULI AZINDUA GHALA LA MITAMBO YA KUHIFADHIA GESI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dk. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri wa Nishati Dk. Medard Kalemani, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Taifa Gas Tanzania Limited Bw. Rostam Aziz na viongozi wengine akikata utepe kuashiria kuzinduliwa kwa Ghala na Mitambo ya Gesi ya LPG vya Kampuni hiyo huko Vijibweni, Kigamboni, jijini Dar es salam leo Juni 25, 2019.
 

NA FARAJA EZRA


RAIS John Pombe Magufuli amezindua Ghala na Mitambo wa kuhifadhia mitungi ya Gesi ya LPG ya Taifa Gas katika kata ya Vijibweni Wilaya ya Kigamboni Mkoani Dar es Salaam.

Aidha Mtambo huo unatumika mahsusi kupokea na kuhifadhi mitungi mbalimbali ya Gesi ili iweze kutumika kwa matumizi majumbani.

Akizungumza katika uzinduzi huo jijini Dar es Salaam Rais Magufuli alisema uwepo wa gesi hiyo ni fursa kwa Watanzania kwa kupata ajira lakini pia kupunguza matumizi ya mkaa majumbani ambayo huleta madhara kwa afya ya watumiaji kwa kuvuta moshi wa mkaa na kupelekea Kansa na TB.

Licha ya madhara hayo inaokoa gharama matumizi ya mkaa kwani gesi hutumika kwa kipindi kirefu, pasi matumizi ya mkaa.

Aidha Rais Magufuli alisema gesi hiyo pia imetengenezwa kwa kutumia Mchanganyiko wa Methen na ethen ambapo huipa upekee wa aina yake katika ubora lakini pia huchukua mda mrefu kuisha.

Alisema sekta ya Nishati na Madini ni muhimu saan katika kuinua maendeleo ya taifa kwa sababu sekta zingine haziwezi kufanya shughuli zake za kimaendeleo bila kutegemea sekta ya Nishati na Madini au Gesi.

Hata hivyo amewataka wawekezaji wa ndani na wa nje kuunga juhudi za serikali katika kuwekeza zaidi katika sekta mbalimbali ili kukuza uchumi wa viwanda ifikapo mwaka 2025.

Alisema kadiri wawekezaji wanapoongezeka nchini ndivyo inavyoondoa changamoto mbalimbali za Ajira licha ya hivyo pia kukuza uchumi wa nchi katika kujipatia fedha za kigeni.

"Ninajivunia kusikia mwekezaji wa Mtambo huu wa Taifa Gas ni mtanzania,, hi inanipa Faraja na Matumaini kuona Watanzania kuwa na uwezo wa kumiliki makampuni tofauti tofauti ili kukuza uchumi wa nchi" alisema Rais Magufuli.


Waziri wa Nishati na Madini Merdard Kalemani..


Alisema Mtambo huu wa Taifa Gas umeanzishwa mwaka 1965 lakini haukuweza kuendelea kutokana na mwekezaji kushidwa kuendeleza ndipo ukafungwa.

Aidha ni jambo lenye matumaini kuona mwekezaji mpya amedhamiria kusukuma gurudumu la maendeleo ili kukuza uchumi wa mtu mmoja mmoja lakini pia Taifa kwa ujumla.

Akimtaja mmiliki wa Taifa Gas ambaye pia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Mtambo huo ni Rostam Azizi akiwakilisha nchi katika viwango vya kimataifa katika sekta hiyo.

No comments:

Post a Comment

Pages