HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 18, 2019

SEKRETARIETI YA MAADILI YA VIONGOZI WA UMMA INAENDELEA MALI ZA VIONGOZI WOTE WA UMMA

1.Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akifungua leo Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.
Kamishna wa  Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma  Jaji Mstaafu Harold Nsekela akitoa elimu  leo wakati wa mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.
Baadhi ya washiriki wa Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora. (Picha na Tiganya Vincent). 
 
 
Na Tiganya Vincent

Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma inaendelea na zoezi la kuhakiki kwa viongozi wote wa Umma wanaojaza fomu za tamko la rasilimali na madeni ili kuepusha mgongano wa maslahi miongoni mwao.

Kauli hiyo imetolewa leo na Kamishna wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Jaji Mstaafu Harold Nsekela wakati wa Mafunzo na maelekezo ya maadili ya siku moja kwa Viongozi wa Umma wa Sekretarieti ya Mkoa wa Tabora na Manispaa ya Tabora.

Aidha Mh Nsekela amewata Viongozi hao kufanya kazi kwa Uadilifu kwa kufuata Sheria ya Maadili ya Viongozi wa Umma namba 13 ya mwaka 1995 ambayo inawataka Viongozi wa Umma kutekeleza Majukumu yao kwa Maslahi ya Taifa.

Alisema lengo ni kutaka viongozi wa umma wafanye kazi kwa kuzingatia maadili na kuweka maslahi ya Taifa mbele badala ya maslahi binafsi.

Mh Jaji Nsekela katika hotuba yake aliongeza kuwa mgongano wa maslahi kwa baadhi ya viongozi wa umma unaweza kulisababisha Taifa hasara ya kuwa na miradi inayotekelezwa chini ya viwango.

Katika hatua nyingine Kamishna huyo wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma aliwataka viongozi wote wanaohusika katika ujazaji wa fomu za tamko la rasilimali na madeni kutenga muda wa kutosha kujaza fomu zao kwa ufasaha.

Alisema mara nyingi Viongozi wanaojaza fomu za tamko la rasilimali na madeni wamekuwa wakisubiri siku za mwisho ndio wanaanza kujaza , jambo ambalo linaweza kusababisha kuachwa baadhi ya mali bila kuorodheshwa katika fomu hiyo ya Tamko.

Aliongeza kwamba Kiongozi wa Umma kujaza fomu za Tamko la Raslimali na Madeni ni takwa la Kisheria na ni lazima wala sio ombi. Na kwamba Kiongozi asipojaza fomu hizo na kuzirejesha kwa Kamishna wa Maadili kwa wakati ni kosa la kimaadili kisheria.

Alifafanua kwamba Kiongozi wa Umma anatakiwa kutoa Tamko lake la Raslimali na Madeni yake kila mwaka ifikapo mwishoni mwa Mwaka yaani tarehe 31 Desemba ya kila mwaka.

Mafunzo haya ya Maadili yamehudhuriwa na Viongozi wa Umma wa Manispaa zaidi ya Tabora zaidi ya 200 wakiwemo Wakurugenzi, Makamanda wa polisi na jeshi la wananchi, wakuu wa wilaya, Madiwani, wakuu wa Idara na Vitengo.s

No comments:

Post a Comment

Pages