Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela na
kapteni wa timu ya mpira wa miguu ya Benki ya CRDB akimtambulisha kwa
Waziri Mkuu Mheshimiwa Kassim Majaliwa mchezaji wa timu Abdul Van
Mohammed wakati timu hiyo ilipocheza na timu ya Bunge FC . Timu ya mpira
wa miguu ya Benki ya CRDB iliifunga timu ya Bunge FC kwa mikwaju ya
penati 3 kwa 1 katika Bonanza lililofanyika Uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB Abdulmajid Nsekela
akionyesha Kombe la Ushindi baada ya kukabidhiwa na Waziri Mkuu
Mheshimiwa Kassim Majaliwa (wa pili kushoto). Timu ya mpira wa miguu ya
Benki ya CRDB iliifunga timu ya Bunge FC kwa mikwaju ya penati 3 kwa 1
katika Bonanza lililofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma.
Wafanyakazi wa Benki ya CRDB wakishangilia ushindi baada ya
kuifunga timu ya Bunge FC kwa mikwaju ya penati 3 kwa 1 katika Bonanza
lililofanyika Uwanja wa Jamhuri Dodoma, mwishoni mwa wiki.
No comments:
Post a Comment