Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji) Mhe. Angellah Kairuki, akitoa hotuba ya ufunguzi wakati wa mkutano wake na wawekezaji kutoka Marekani waliopo nchini alipokutana nao 17 Juni, 2019 katika Ukumbi wa Mikutano wa Hyatt Jijini Dar es Salaam ili kujadili masuala ya uwekezaji nchini.
NA MWANDISHI
WETU
Waziri wa Nchi Ofisi ya
Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Uwekezaji Mhe. Angellah Kairuki
amewahakikishia wawekezaji kutoka Marekani uwepo wa mazingira rafiki ya
uwekezaji nchini kwa kuzingatia mchango wao katika masuala ya uwekezaji.
Ametoa kauli hiyo wakati
akifungua kongamano la siku moja la kujadili masuala ya kuboresha mazingira ya
biashara pamoja na uwekezaji nchini lililofanyika tarehe 17 Juni, 2019 katika
Ukumbi wa mikutano wa Hyatt Jijini Dar es Salaam.
Mazungumzo hayo yaliyolenga
kujadili changamoto zinazowakabili na kujadili namna bora ya kukabiliana nazo
na hatua mahsusi ambazo Serikali imeendelea kuzichukua ili kuboresha mazingira
ya biashara na uwekezaji.
Kongamano hilo limeandaliwa
na Ubalozi wa Marekani kwa kushirikiana na Chemba ya Wafanyabiashara wa
Kimarekani nchini Tanzania na kuhusisha
wawakilishi wa Kampuni 47 kati ya 238 za Kimarekani na
kuhudhuriwa na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Profesa
Palamagamba Kabudi, Maafisa Waandamizi wa Serikali ya Tanzania, Wawakilishi wa
Ubalozi wa Marekani pamoja na Wanachama wa Jumuiya ya Wafanyabiashara wa
Kimarekani.
Waziri Kairuki alieeleza
nia ya Serikali ni kuendelea kuwa na mazingira wezeshi yanayowavutia wawekezaji
nchini katika kuendelea kuchangamkia fursa zilizopo na kupokea maoni yao ili
kutatua changamoto wanazokumbana nazo.
“Serikali itaendelea kuweka
mkazo mkubwa wa maboresho katika maeneo mbalimbali yatakayo kuvutia wawekezaji
ikiwani pamoja na uboreshwaji wa sekta
ya mawasilino, miundombiu ya barabara na usafirishaji ili kuwa na mazingira
mazuri ya wawekezaji kuja kuwekeza nchini,”alisema Waziri Kairuki.
Aliongeza kuwa ifikapo
mwezi Julai mwaka huu, serikali itaanza kutekeleza Mpango Kazi wa Uboreshaji wa
Mazingira ya Biashara na Uwekezaji ambao tayari umefanyiwa maboresho na
utekelezaji wake utaanza mapema mwaka ujao wa fedha wa 2019/ 2020.
Aidha waziri aliahidi
kuendelea kusimamia maeneo muhimu ikiwemo ushiriki wa sekta binafsi katika
maeneo ya uwekezaji na kueleza maboresho haya yatatekeleza hasa katika
kuboresha mifumo na kuwa na maziringa mazuri yanayotabirika kwa wawekezaji.
“Kwa kutambua umuhimu wa
Sekta binafsi, tutaendelea kusimamia ushiriki wao kikamilifu ili kuleta tija pasipo
kubagua sekta hiyo na kuendelea kuwa na mifumo inayotabirika kwa ajili ya
wawekezaji.
Naye Waziri wa Mambo ya Nje
na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi alifafanua
kuwa, jitihada za Serikali ni kuhakikisha kunakuwa na mahusiano mazuri ya
kidiplomasia baina ya nchi hizo mbili kwa kuzingatia zote zinategemeana katika
masuala hayo ya uwekezaji.
“Kimsingi tunapaswa kuwa na
uelewa wa pamoja kuwa, Tanzania na Marekani zinategemeana katika masuala haya
ya uwekezaji kwani mnatuhijai na sisi tunawahitaji hivyo lazima tukae meza moja
na kuyajenga endapo tunaona kuna maeneo ya kuboresha yenye tija ya kuendeleza
mahusiano mazuri yaliyopo ni vyema tukayafanyia kazi pamoja”, Alisistiza Profesa
Kabudi.
Kwa upande wake Kaimu
Balozi wa Marekani nchini Dkt. Inmi Patterson katika hotuba yake ya ufunguzi
alieleza kuwa, majadiliano hayo ni mwanzo mzuri wa kuendelea kutekeleza
mabadiliko ya kisera yatakayosaidia kuongeza uwazi na mazingira rafiki ya
ufanyaji wa biashara nchini.
“Majadiliano ya leo ni
mwanzo wa utekelezaji wa mabadiliko ya kisera yatakayoongeza uwazi na kuboresha
mazingira ya kufanya biashara na tunaunga mkono jitihada hizi za Serikali ya
Tanzania kwa kuzingatia mahusiano mazuri yaliyopo sasa,”Alieleza Kaimu Balozi Patterson.
Aliongezea kuwa Serikali ya
Marekani itaendelea kuunga mkono ushiriki wa sekta binafsi katika jitihada za
maendeleo nchini humo kupitia ubia kati ya sekta binafsi na sekta ya umma
(Public private partnerships) ambao utaimarisha mazingira ya kibiashara na
ubunifu ambao utanufaisha Wananchi wa Tanzania.
Aidha alieleza kuwa nchi
yake imeendelea kuwa mstari wa mbele katika uwekezaji, kwa kuzingatia Takwimu
za Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Wafanyabiashara wa Kimarekani wamewekeza
zaidi ya Dola za Kimarekani bilioni 4.7 nchini Tanzania na kuzalisha takriban
nafasi za ajira 52,000 katika kipindi cha miaka 28 nchini kote Tanzania.
No comments:
Post a Comment