HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

June 25, 2019

Wafanyakazi Tarura wafariki kwa ajali ya gari Iringa


 Picha zikionyesha ajali ya gari dogo aina ya Toyota Hilux mali ya Tarura yenye namba za kusajili STL 3807 na Fuso lenye namba za usajili T 146 BAZ  mali ya Wilson Msenga. Ajali hiyo ilitokea katika Tarafa ya Isimani mkoani Iringa.


Na Datus Mahendeka, Polisi Iringa

Wafanyakazi wawili wa Tarura Mkoa wa Songwe wamefariki kwa ajali ya uso kwa uso wakitokea Mkoa wa Iringa wakielekea Dodoma.

Waliofariki ni Lodrick Richard, miaka 35, kabila Mchaga mkazi wa Dar es Salaam ambaye ni dereva wa gari waliokuwa wakisafiria pamoja na Joyce Enezer, miaka 45, kabila Mchaga mkazi wa Moshi.

Akizungumza na waandishi wa habari Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Kamishna Msaidizi wa Polisi Juma Bwire amesema ajali hiyo imetokea Juni 25 majira ya saa 11:45 alfajiri.

"Wafanyakazi hawa waliokuwa wanaenda Dodoma kikazi ambapo walipofika maeneo ya Izazi Tarafa ya Isimani wakiwa kwenye gari lenye namba za kusajili STL 3807 aina ya Toyota Hilux mali ya Tarura walikutana na Fuso.

Kwa mujibu wa Kamanda Bwire, Fuso hilo lenye namba za usajili T 146 BAZ  mali ya Wilson Msenga likiendeshwa na mtu kwenye jina moja la Amos ambalo lilikuwa likitokea Dodoma kuja Iringa  ambapo waligongana uso kwa uso ambao miili yao imekabidhiwa kwa Meneja wa Tarura Manispaa ya Iringa ili kupelekwa Dodoma kwa tararibu zingine.

Aidha alitaja majeruhi wa ajali hiyo kuwa ni  Ernest Mgeni, miaka 49, kabila Mkinga, Gervas Myovela, miaka 44, kabila Mhehe na Jamadin Mikata, miaka 32 wote wakazi wa Mbozi ambao wamelazwa katika Hospitali ya Rufaa Iringa kwa matibabu.

Alisema dereva wa Fuso anatafutwa baada ya kulimbia mara baada ya ajali hiyo, kutokana na uzembe wake wa kuhama upande wake wa barabara.

No comments:

Post a Comment

Pages