*Azivunja Jumuiya
za watumiaji maji Hedaru
*Aagiza Katibu wa
Jumuiya moja akamatwe
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimsikiliza Mhandisi wa Maji Wilaya ya Same Mussa Msangi, wakati akikagua mradi wa maji wa Lengeni-Hedaru, wilayani Same kabla ya kuuzindua, Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akizindua mradi wa maji wa Lengeni-Hedaru, wilayani Same, Julai 19.2019. Tokea kushoto ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Same, Anne Shija, Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro, Anna Mghwira, Mwenyekiti wa (CCM) Mkoa wa Kilimanjaro, Patric Boisafi, Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Awesu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, akimtwisha ndoo ya maji Mkazi wa Hedaru, Mary Fue, baada ya kuzindua mradi wa maji wa Lengeni-Hedaru, uliyopo wilayani Same, Julai 19.2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).

WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amemsimamisha kazi
Mhandisi wa Maji wa Wilaya ya Same, Mussa Msangi kwa kosa la kumdanganya kuhusu
mradi wa maji aliouzindua leo katika kata ya Hedaru.
Amechukua uamuzi huo leo jioni (Ijumaa, Julai 19,
2019) wakati akizungumza na mamia ya wakazi wa Hedaru mara baada ya kuzindua
mradi wa maji wa Lengeni-Hedaru, wilayani Same.
Waziri Mkuu alibaini kuwepo kwa tatizo wananchi
walipoanza kuzomea wakati zikitolewa salaam za utambulisho kwa viongozi
alioambatana nao. Kabla hajahutubia, aliamua kumuita Mhandisi huyo aelezee
ukweli wa madai ya wananchi kwamba maji yametoka leo kutokana na ujio wake.
"Eleza ni kwa nini nilipofungua maji, hayakuwa
na presha ya kutosha na wewe umesema upatikanaji wa maji umefikia zaidi ya
asilimia 80?"
Alipoulizwa kwa mwezi wanakusanya kiasi gani cha
fedha kutokana na mauzo ya maji hayo, Mhandisi Msangi alijibu kwa mwaka
uliopita walikusanya sh. milioni saba tu.
"Haiwezekani kama maji yanatoka, wenye KAMATI
wapate shilingi milioni saba. Ni ama maji hayatoki au wanakusanya hela na
wanazila."
Alipoambiwa aelezee utendaji wa mradi huo wa maji na
kama alikuwa akiufuatilia, alishindwa kutoa maelezo kamili, akidai kuwa leo
maji yanatoka kidogo kwa sababu kuna hali ya mawingu. "Mbona kule ndani
ulisema zile betri zinasaidia kuvuta maji na kubalance upatikanaji wa maji
wakati hakuna jua la kutosha?" alihoji Waziri Mkuu.
Waziri Mkuu aliamua kumuita mwenyekiti wa Jumuiya ya
watumiaji maji au Kiongozi mwingine yeyote aje atoe maelezo, lakini wote
hawakuwepo kwenye mkutano huo. Ndipo akachukua uamuzi wa kuzivunja jumuiya
hizo.
"Jumuiya zote za maji nazivunja kuanzia
leo, na wahusika wote watafutwe na Jeshi la Polisi. Haiwezekani nipewe kazi ya kuzindua
mradi ambao hauna maji," alisema Waziri Mkuu.
"Katibu Tawala wa Mkoa lete wakaguzi wa
mahesabu kwenye huu mradi, pia leta Mhandisi mwingine asimamie huu mradi. Huyu
arudishwe kwa Waziri wake," alisema.
Waziri Mkuu pia alimwagiza Naibu Waziri wa Maji,
Jumaa Awesu abaki Hedaru na afuatilie utendaji wa mradi huo kisha ampe taarifa.
Wakati akimaliza kutoa maagizo hayo, Katibu wa
Jumuiya ya watumiaji maji Hedaru-Masasi (HEWAUA), Bw. Francis Kazen Kiondo
aliletwa akiwa chini ya ulinzi wa polisi, lakini Waziri Mkuu alielekeza
apelekwe kituoni akatoe maelezo.
Taarifa zilizothibitishwa zimebainisha kuwa Kata ya
Hedaru inazo Jumuiya tatu za watumiaji maji ambao ni Hedaru-Masasi, Lung wana
na Mradi wa Kati. Wakazi wa Hedaru wanakadiriwa kufikia 20,000.
Ilibainika kwamba wiki iliyopita, Mwenyekiti wa
Hedaru-Masasi, Bw. Clement Ngoka aliamua kujiuzulu nafasi hiyo kwa sababu ya
upinzani aliokuwa akipata kwa viongozi wenzake ambao pia wanadaiwa
kuwaunganishia maji baadhi ya watu hadi majumbani kwao na fedha zilizolipwa
hazijulikani zilipoenda.
Awamu ya pili ya mradi wa maji alioenda kuuzindua
Waziri Mkuu, inahusisha ujenzi wa chanzo cha maji katika korongo la mto Rangeni
ambao ulikamilika Desemba 2018. Chanzo hicho cha mtiririko, kilitarajiwa
kuzalisha lita 750,000 kwa siku ili kusaidia maji yanayozalishwa kwenye visima
ambayo yana ujazo wa lita 7,500 kwa saa.
IMETOLEWA NA:
OFISI YA WAZIRI
MKUU,
IJUMAA, JULAI 19,
2019.
No comments:
Post a Comment