HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 03, 2019

Benki ya Posta yawaita wananchi kutembelea banda lao sabasaba kupata huduma

Meneja wa Biashara za Kieletronik Benki ya Posta Tanzania, Amina Mohamed, akizungumza na Waandishi wa habari (hawapo pichani) katika banda la benki hiyo.







Na Janeth Jovin

BENKI  ya Posta Tanzania imewataka wananchi kutembelea banda lao lililopo katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara kwa lengo la kupata huduma mbalimbali za kibenki  pamoja na kujifunza jinsi programu maalum ya kuuza,kununua na kutangaza kwa njia ya kimtandao  inavyofanya kazi.

Akizungumza jijini Dar es Salaam leo katika Viwanja vya maonyesho ya 43 ya Kimataifa ya Biashara,Meneja wa Biashara za kielektroniki wa Benki hiyo, Amina Mohamed  anaema wananchi wakifika katika banda hilo wataweza kupata huduma za kibenki.

Aidha anasema benki hiyo imekuja na mfumo huo mpya wa kuuza, kununua na kutangaza kwa njia ya mtandao kwa lengo la kuwapa fursa  wafanyabiashara kuuza biashara zao kimtandao zaidi.

Anasema wamejipanga kufanya biashara kimtandao na kwa kushirikiana na makampuni mbalimbali ya simu na kulipia kimtandao katika huduma ya Paypal na hii ni kuhakikisha wanaenda sambamba na ukuaji wa teknolojia nchini.

"Mjasiliamari wowote anaweza kujiunga kupitia website au kufika katika maduka yetu ili kujiandikisha katika kutumia huduma hiyo kwa kutangaza, kununua na kuuza bidhaa mbalimbali," alisema Mohamed.

Aidha anasema sababu iliyowafanya kuingia katika uuzaji wa bidhaa kwa njia ya kimtandao ni kutokana na vijana wengi kutumia mtandao na kuona biashara  nyingi kwa sasa  zinauzika kwa wingi.

"Tunaona biashara nyingi sasa zinauzika kimtandao na sisi tumeamua kuzindua Posta shop Tanzania na hii in kuhakikisha tunawafikia watu wote kwa wakati mmoja," alisema

Mohamed anasema  kwa mwaka huu maonyesho hayo yamekuwa na muamko mkubwa kutokana na makampuni mengi kushiriki pamoja na wajasiriamali wengi kujitokeza .


No comments:

Post a Comment

Pages