Na Tatu Mohamed, Dar es Salaam
NAIBU
Waziri wa Maliasili na Utalii, Constantino Kanyasu, amewaalika
wawekezaji kutoka katika mataifa mbalimbali kuwekeza katika hifadhi za
mazingira asilia kote nchini.
Uwekezaji huo ni katika ujenzi wa miundombinu, hoteli, kambi za utalii, vituo vya utafiti, utalii wa parachuti na mwingineo
Akizungumza
katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa Dar es Salaaam
(DTIF), Kanyasu amesema lengo ni kuhakikisha mtalii anapoingia hifadhini
anapata huduma zote muhimu
"Serikali
tumeamua kuwekeza nguvu katika hifadhi zetu zote zinazobeba misitu,
tumejipanga kujenga miundombinu madhubuti na ndio maana tumewaalika
wawekezaji waje sasa, wajenge mahoteli.
"...na
tunataka hata huduma za kibenkina nyingine zote ziwepo ili mtalii
anapoingia hifadhi asihangaike tena kwenda kutafuta huduma nje, tunataka
akifika msitu apate chakula, alale apate huduma za kifedha," amesema
Kanyasu
Ameongeza kuwa uboreshaji wa Ikolojia katika hifadhi hususani za misitu ni muhimu katika kuhamasisha utalii
Pia
Kanyasu amesema katika msimu wa maonyesho hayo, Wakala wa Huduma za
Misitu Tanzania (TFS) imeandaa safari za utalii kwa washiriki na ambao
watafika katika maonyesho hayo kwa kuwapeleka katika hifadhi ya
mazingira asilia ya Maghamba iliyopo Lushopo mkoani Tanga kuanzia Julai
12 hadi 14 mwaka huu.
Mbali
na hayo, Kanyasu amesema serikali imeweka mkakati wa kuhuisha mashamba
yote ya hifadhi za misitu yaliyokuwa yameshaharibiwa.
No comments:
Post a Comment