Na Janeth Jovin
WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetoa fursa kwa watanzania kufanya safari ya utalii ndani ya hifadhi ya Mazingira asilia ya Magamba iliyopo mkoani Tanga.
Akizungumza na waandishi wa habari leo katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara Ofisa Utalii, Mafunzo na utafiti katika hifadhi hiyo, Samiji Mlemba (pichani) anasema safari ya kuelekea katika hifadhi hiyo itaanza Julai 12 katika viwanja vya sabasaba mahali ambapo maonesho yanafanyika na Julai 14 mwaka huu watu watarejea.
Anasema watu watakaombelea hifadhi hiyo wataona vitu mbalimbali ikiwamo handaki ambalo Wajerumani walilitumia katika Vita ya kwanza ya dunia, mabaki ya majengo ya kijerumani pamoja na kuliona eneo maarufu linaloitwa jiwe la Mungu.
"Tukiwa magamba pia tutapata bahati ya kushuhudia maji mazuri, ndege kama usambara liver, kipepeo, mbega. Hali ya hewa ya magamba ni nzuri Sana watu hawatajutia kwenda huko hivyo wajitokeze kwa wingi wala wasisite.
Jinsi ya kufanikisha Safari kila mmoja atapaswa kuchangia ambapo watu wakubwa watalipa kiasi cha Sh. 171,000 na watoto Sh. 148,000 , kiasi hichi cha fedha ni gharama ya Chakula, usafiri, maradhi, ngoma za asali, gharama za utembeaji ndani ya hifadhi na za muongoza utalii," anasema.
Hata hivyo Milemba amewataka wananchi kufika katika banda la Maliasili walipo TFS ili kupatiwa maelekezo ya jinsi ya kujisali ili waweze kwenda katika Safari hiyo.

No comments:
Post a Comment