HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 09, 2019

Mafundi viyoyozi na majokofu watakiwa kusoma VETA

Na Janeth Jovin

MAMLAKA ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA),imewataka mafundi wa majokofu na viyoyozi kusoma katika mamlaka hiyo kwa lengo la kufundishwa  njia sahihi ya kufanya ukarabati wa vifaa hivyo bila kuharibu Mazingira.

Akizungumza katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara maarufu sabasaba, Mwalimu wa Chuo hicho kutoka Chang'ombe ,Daudi Kadinda anasema Kutokana na uharibifu wa mazingira unaofanywa na mafundi hao wamekuja na teknolojia mpya itakayosaidia kutunza mazingira.

Anasema uharibifu mkubwa unaofanywa na mafundi hao ni pale wanapobadilisha gesi Kutoka katika jokofu au kiyoyozi kilichoharibika kwa lengo la kutengeneza.

"Teknolojia hii ni ya kutunza mazingira bila kumwaga gesi unajua wanapofanya ukarabati na kumwaga gesi ni kitu hatari katika mazingira kwani gesi ile uenda juu na kusamba angani na kupanda  kwenda katika anga kisha kutoboa tabaka la juu ambalo utoa mwanga wa jua moja kwa moja," alisema na kuongeza

"Mwanga huo unaposhuka chini nakuwakumba watu usababisha kansa ya ngonzi, ukame mimea lakini pia watu wanapata magonjwa kama saratani," anasema

Aidha Kadinda anasema mafundi hao wanaweza kufanya ukarabati kwa njia mbadala kwa kunyonya gesi iliyomo kwenye jokofu au kiyoyozi kilichoharibika na kuweka katika kwenye mtungi mwingine wa gesi.

Anasema kifaa hicho kinaitwa Refrigent recover unit  inarahisisha kubadilisha gesi kwa usalama zaidi bila kumwaga gesi .

"Pia teknolojia hii inasaidia kuhifadhi gesi na ikimalizika kukarabati kuirudishia katika jokofu au kiyoyozi kilichoharibika na kuendelea kutumia," anasema.

No comments:

Post a Comment

Pages