HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 03, 2019

Makamu wa Rais azitaka taasisi kusitisha uagizaji wa bidhaa za samani kutoka nje

 Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan akimkabidhi tuzo ya kipingele cha wadhamini, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya CRDB, Abdulmajid Nsekela, wakati wa uzinduzi wa Maonyesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya 43 (DITF). (Picha na Francis Dande).
 Makamu wa Rais akipata maelezo katika banda la JKT.
 Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika uzinduzi wa maonyesho ya Sabasaba.
 Baadhi ya washiriki kutoka nje ya nchi.


Na Janeth Jovin

MAKAMU wa Rais, Samia Hassan Suluhu amezitaka taasisi za Serikali kusitisha uagizaji wa bidhaa za samani kutoka nje ya nchi kama agizo hilo lilivyotolewa hapo awali.

Akizungumza katika uzinduzi wa maonyesho ya Kibiashara ya Kimataifa ya 43 (DITF), Samia amesema Serikali ilikwishatoa maelekezo ya kusitisha uagizaji wa bidhaa hizo za samani kutoka nje ya nchi.

"Serikali tayari ilikwishatoa maelekezo ya kusitisha uagizaji wa bidhaa za samani zote za nje ya nchi naomba kurudia na kusisitiza tena kuwa wizara na taasisi zote zizingatie agizo hili katika manunuzi yao,"anasema Samia.

Anasema  ili ujenzi wa uchumi wa viwanda ushike kasi ya kutosha hakuna budi kwa sekta kama vile kilimo mifugo, uvuvi na madini kutoa malighafi za kutosha viwanda hivyo.

Samia anasema wakati wanahimiza uchumi wa viwanda msukumo uliwekwa kwenye viwanda vinavyozalisha malighafi vya hapa nchini.
Aliiagiza wizara ya viwanda kuhakikisha inadhibiti kuingia kwa bidhaa zisizo na ubora kutoka nje na kufanya jalala ili kuzipa nafasi bidhaa za ndani.

Anasema ni vyema ikahakikisha kwamba bidhaa zinazotoka nje  na kuingizwa ndani zinakuwa ni zile zenye ubora tu ambazo zina uwezo wa kuleta changamoto kwa bidhaa za ndani.

"Tuna uwezo wa kuzalisha bidhaa bora zinazokidhi mahitaji ya soko la ndani lakini changamoto ni kuwepo kasumba ya Watanzania kupenda kutumia bidhaa za nje kuliko za ndani ilhali bidhaa zetu zina ubora unaljitosheleza," alisema Samia.

Anasema wanachohutaji ni kuhakikisha Wizara ya Viwanda inasimamia wazalishaji kuongeza thamani na kuboresha zaidi bidhaa zetu kuwa za kisasa ili ziuzwe na nje.

Anasema baada ya bidhaa kuongezewa thamani balozi za Tanzania nje ya nchi zitapata kazi ya kutafuta masoko.

Aliziagiza mamlaka zinazohusika na upatikanaji wa malighafi kuhakikisha zinazalisha malighafi zitakazokidhi mahitaji ya viwanda vya ndani.

Anasema kwa kufanya hivyo Viwanda vya ndani vitakuwa na uhakika wa soko la ndani na nje, na kusaidia kuongeza akiba fedha za kigeni.

Pia aliziagiza mamlaka zinazohusika kusimamia utekelezaji wa mpango wa kuboresha mfumo wa udhibiti wa biashara nchini (Blueprint) ikiwamo Shirika la Viwango Tanzania (TBS),  Mamlaka ya Chakula na Dawa (TFDA, ) Mamlaka ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali (GCLA), Wizara ya Mifugo na Uvuvi na Wizara ya Maliasili na Utalii kusimamia utekelezaji wake.

"Mamlaka husika zisimamie kwa nguvu zote utekelezaji wa Blueprint na tutazisimamia kwelikweli kuhakikisha zinaleta mrejesho mara kwa mara wa udhibiti wa vikwazo vya biashara ili pale penye tatizo tuwe tunalishughulikia," alisema Samia.

Naye Waziri wa Viwanda na Viashara Innocent Bashungwa, anasema wapo katika mkakati wa mapitio ya sera ambayo yataendana na uchumi wa Viwanda na kukamilika kufikia 2020.

Anasema muitikio wa maonyesho hayo kwa mwaka huu umeongezeka na idadi ya makampuni ya nje yaliyoshiriki kufikia 580 kutoka 508 mwaka jana.

No comments:

Post a Comment

Pages