Na Faraja Ezra
BARAZA la Michezo ya
Majeshi Duniani (CISM) linatarajia kushiriki Michezo ya Riadha, Ngumi,
na Mieleka Octoba 18 hadi 27 mwaka huu nchini China.
Michezo ya cism imeanzishwa kwa lengo la kueneza amani na upendo duniani badala ya vita hususan katika nchi korofi.
Akizungumza
na waandishi wa habari Makao Makuu ya Jeshi jijini Dar es Salaam
Mwakilishi wa Baraza hilo kutoka nchini Ubelgiji Kanali Joseph Bakari
alisema Jeshi linashiriki Michezo kama sehemu ya utekelezaji wa kazi
ndani na nje ya nchi.
Aidha
Kanali Joseph alisema pia mchezo huo utahusisha bara nne ikiwemo
Afrika, Asia, Amerika na Ulaya ambapo bara la Afrika watatoa washiriki
47, Asia 32, Ulaya 42 na Amerika 30.
"Miongoni
mwa Michezo itakayochezwa ni pamoja na mpira wa miguu, Ngumi, Golf na
Judo, ikiwa na lengo la kudunisha amani na upendo katika nchi
wanachama,"alisema Kanali Joseph.
Hata
hivyo Kanali Joseph alisema wamekuwa wakikabiliana na changamoto
mbalimbali tangu kuanzishwa kwa baraza hilo ambapo alisema mmoja ya
changamoto ni ushiriki hafifu kwa wachezaji kwa kuwa na uhaba wa elimu
juu ya umuhimu wa cism.
Kanali
Joseph alisema Cism ilianzishwa mnamo mwaka 1948 ambapo mwaka 1979
Tanzania ilifanya vizuri katika Michezo ya Riadha na Ngumi.
Pia
katika Michezo hiyo ikihudhuriwa na viongozi mbalimbali wa serikali na
huku Mgeni rasmi atakuwa Raisi wa Jamhuri ya watu wa China.
Alisema
ni fursa ya pekee kwa Tanzaniaw kushiriki Michezo hiyo ili kupata
uzoefu katika Michezo na kujipatia Ubunifu katika suala la Michezo.
duniani.
No comments:
Post a Comment