MTANZANIA
George Ulaya (pichani), amebuni mtambo wa kufua umeme unaotumia upepo wenye Watt
50,000 ambao utatumika kuendesha viwanda na matumizi ya umeme katika
kijiji kizima.
Ulaya
akiwa chini ya Tume ya Taifa ya Sayansi na teknolojia (COSTECH) aliweza
kuelezea jinsi alivyoanza kwa ubunifu huo akiwa Sumbawanga na sasa
anasambaza teknolojia hiyo katika mikoa mbalimbali nchini.
Akiwa katika viwanja vya maonesho
ya 43 ya kimataifa ya biashara ya Dar es salaam (DITF) yanayofanyika
katika viwanja vya Mwalimu Julius Nyerere, Ulaya ambaye yuko katika banda
la COSTECH amesema alianza na kutengeneza mashine ya kufua umeme kwa
njia ya upepo wa Watt 300 lakini kwa sasa baada ya kuwezeshwa na Tume ya
Sayansi ameendelea na kutengeneza mashine ya kisasa inayotoa Watt
50,000.
"Nawashukuru
COSTECH baada ya mwaka 2010 kunipa tuzo ya ubunifu huu na kunisaidia
sasa nimepaa nipo kiteknolojia zaidi kwa maana natumia nyenzo mbalimbali
za kisasa na nimekuwa mbunifu mkubwa wa kutengeneza mashine
mbalimbali," amesema Ulaya.
Amesema kupitia mashine hiyo umeme wake unatumika katika kijiji kizima na hata upepo ukikatika umeme unaendelea kuwaka.
"Mashine
hii ni gharama nafuu, pia itasaidia kwenye uchumi wa viwanda kwasababu
watu wanatumia umeme kuendesha shughuli zao mbalimbali," amesisitiza.
No comments:
Post a Comment