Wakili wa
Serikali Mwandamizi, Edna Kamara, akizungumza na waandishi wa habari
kwenye viwanja vya Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF)
maarufu Sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere Barabara ya Kilwa jijini Dar es Salaam.
Na Tatu Mohamed
IMEBAINISHWA
kuwa Taasisi za kidini, vyama vya siasa na klabu za mpira wa miguu
ndizo zinaongoza katika kulipa marejesho ya mwaka kwa wakala wa Usajili,
Ufilisi na Udhamini (RITA), ukilinganisha na taasisi nyingine.
Hayo
yamesemwa na Wakili wa Serikali Mwandamizi, Edna Kamara kwenye
viwanja vya maonyesho ya 43 ya biashara ya Kimataifa (DITF) maarufu
sabasaba yanayoendelea kwenye viwanja vya mwalimu Nyerere barabara ya
Kilwa jijini Dar es Salaam.
Kamara
amezitaka taasisi nyingine ambazo zinasuasua kulipa ada ya marejesho ya
kila mwaka kwa kuzingatia sheria ya kulipia kwa tarehe husika ambayo
bodi imesajiliwa ili kuepuka adhabu za kisheria zikiwamo faini.
Amefafanua
bodi ya wadhamini inatakiwa kufanya mrejesho kila mwaka tarehe husika
kwa kujaza fomu namba T.1.5 na kulipia ada ya Sh 50000 kwa mujibu wa
sheria ya muunganisho sura ya 318 toleo 2002 kuepuka kulipa faini ambapo
wasipofanya hivyo watalazimika kulipa faini.
"Hapa
kwenye maonyesho tunatoa huduma hii, hivyo ambao wataona uvivu kufika
ofisini kwa ajili ya kulipia wake hapa" amesema Kamara.
Amesema vyama vya siasa ambavyo vinasuasua kulipa ada hii vitabanwa na sheria ya uchaguzi unaokaribia.
No comments:
Post a Comment