HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 07, 2019

Mkurugenzi Wizara ya uvuvi aeleza jinsi mtambo wa kukausha dagaa tani moja kwa nusu saa utakavyowanufaisha wavuvi

Na Janeth Jovin

MKURUGENZI msaidizi wa Huduma za Ugani kutoka Wizara ya Mifugo na Uvuvi, Antony Dadu, amesema kuwa teknolojia mpya  ya mtambo utakaoweza kukausha dagaa tani moja kwa nusu saa unaelezwa kuwa ni mkombozi kwa wavuvi.

Dadu ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati wa mkutano wa ana kwa ana ya Biashara (B2B) katika sekta ya maliasili na mifugo uliyofanyika katika viwanja vya Maonesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa maarufu sabasaba.


Anasema mtambo huo umebuniwa na kufanyiwa utafiti daktari mmoja baada ya kugundua wavuvi wanapata shida hasa katika manunuzi ya samaki.

Akizungumza na Wafanyabiashara, Wafugaji na Wakulima mbalimbali, . Dadu amewataka watanzania kuwa mstari wa mbele kuchangamkia fursa katika sekta ya Uvuvi kwani imekuwa na faida kubwa kwa kutengeneza kipato kitakachokusaidia kuinuka kiuchumi.

“Tunahamasisha watu waweze kujiunga katika uvuvi kwenye bahari kuu ili kumuwezesha kupata kipato kwa maendeleo na ukuaji wa uchumi. Jaribuni kutengeneza teknolojia ambayo itakuwa inafaida katika sekta ya Uvuvi ili kuweza kukufanya unufaike, gereji za meli hapa Tanzania hakuna mpaka Mombasa ndo ipo hivyo jaribuni kutengeneza teknolojia mbayo ityaweza kufanya hivyo”. Anasema  Dadu.

Aidha Dadu ameongeza kuwa ufugaji wa Samaki kwenye vizimba unaweza kuwasaidia kupata kipato kikubwa na wakawa wafanyabiashara wakubwa katika uuzaji wa samaki.

No comments:

Post a Comment

Pages