HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 04, 2019

OLE NASHA –COSTECH SIMAMIENI WABUNIFU KUPATA HAKI MILIKI

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha, akiangalia vitabu mbalimbali vya kufundishia alipofanya ziara katika banda la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwenye Maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha, akiwa katika banda la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwenye Maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba.
Mkufunzi Mtaalamu Elimu Maalum, Hadija Salum, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Mhe. William Ole Nasha, alipofanya ziara katika banda la Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) kwenye Maonyesho ya Sabasaba. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa TET, Dk. Aneth Komba.
Mgunduzi wa Mfumo wa Jua kwa ajili ya kufundishia shuleni, Ernest Maranya, akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. William Ole Nasha.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akipata maelezo kutoka kwa Safia Hashimu Makame mjasiriamali aliyenufaika na mojawapo ya tafiti ya Kilimo cha mwani iliyofanywa na Chuo Kikuu Dar es Salaam kutoka katika Taasisi ya Sayansi za Bahari iliyopo Zanzibar katika Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF) sabasaba.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akiwa katika banda la Chuo Kikuu Dar es Salaam.
 Mmoja wa washiriki wa Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF), akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia katika banda la Chuo Kikuu Dar es Salaam.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akifafanua jambo alipotembelea Banda la Hospitali ya Taifa Muhimbili. Kushoto ni Baraka Ndiege kutoka MUHAS.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akifurahia jambo alipokuwa akiangalia 'nywele bandia' ambazo ni zao la kazi za wajasiriamali wanaopata mafunzo kutoka Chuo Kikuu Mzumbe alipofanya ziara katika banda la chuo hicho Sabasaba.
 Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akitembea katika viwanja vya Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akitembea katika viwanja vya Maonyesho ya 43 ya Biashara ya Kimataifa (DITF).
Naibu Waziri akiwa katika banda la Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania.
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akiwa katika banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia.
  Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha, akipata maeleo kutoka kwa Magreth Tadei wa MUHAS wakati wa ziara yake katika banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia.


          Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknoolojia Mhe. William Ole Nasha ameagiza  tume ya  Sayansi Nchini kusimamia wabunifu kupata haki ya umiliki wa bunifu  zao.

Amesema hayo jijini Dar es salaam, katika viwanja vya sabasaba, Banda la VETA  alipotembelea mabanda ya taasisi zilizo chini ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia walioshiriki katika maonyesho ya 43 ya biashara ya kimataifa (DITF) sabasaba.

Ole Nasha amesema hayo kufuatia mmoja wa wabunifu katika  banda hilo VETA kuomba serikali imtambue rasmi kwani kwa sasa  haki miliki ni ya ubunifu wake wa nyenzo ya kufundishia  mfumo wa sayari mashuleni uko kwa ubia kati yake na VETA hali ambayo Waziri amesema si sawa , haki ya ubunifu huo ni yaaliebuni apatiwe haki yake.

Waziri Ole Nasha amewapongeza VETA kwa kazi nzuri za kukuza ubunufu na ujuzi na kuwataka kusimamia kukuza bunifu mbalimbali za wanafunzi na kuhakikisha zinaingia katika soko ili kusaidia kutatua changamoto mbalimbali za kijamii na kuwapongeza kwa kupata ushindi ambapo VETA ni mshindi wa Tatu wa Jumla katika maonesho hayo.

 Katika hatua nyingine akiwa katika Banda la Tume ya Sayansi na Teknolojia Nchini COSTECH amewaagiza Tume hiyo kuhakikisha wabunifu mbalimbali  wanatambuliwa na kupatiwa haki miliki ya bunifu au ugunduzi waliofanya. Na pia kuendelea kuwafadhili ili kukuza bunifu hizo.

“ maelekezo yangu kwa  COSTECH  ni kuhakikisha ubunifu mbalimbali tuliona hapa sabasaba katika mabanda yetu hauishii katika maonesho , bunifu zikuzwe na tumieni nafasi hii ya maonesho  kuwakutanisha wabunifu na wafanya biashara kwa ajili ya uzalishaji”,

Ole Nasha ametembelea mabanda  ya Taasisi nane zilizo chni ya Wizara ya Elimu , ikiwemo Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu Mkwawa, Chuo Kikuu cha Afya  na Sayansi Shirikish Muhimbili(MUHAS), Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam,  Chuo Kikuu Mzumbe,  Tume ya Atomiki nchini (TAEC) , Tume ya Sayansi na Teknolojia(COSTECH) , Taasisi ya Eimu (TIE) na Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya  na ametumia nafasi hiyo kuwapongeza taasisi zote zilizoshiriki  na kipekee walioweza kupata Ushindi.

No comments:

Post a Comment

Pages