Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akisalimiana na Balozi
wa Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Doanh, ofisini kwa Waziri Mkuu,
Magogoni jijini Dar es salaam, Julai 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri
Mkuu).
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na Balozi wa
Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Doanh, ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni
jijini Dar es salaam, Julai 3, 2019. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu).
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
MKUU, Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa
Vietnam nchini, Mhe. Nguyen Doanh ambapo amewakaribisha wafanyabiashara
kutoka Vietnam waje nchini kuwekeze katika sekta mbalimbali ikiwemo ya
viwanda.
Amesema
Rais Dkt. John Magufuli ameanzisha Wizara ya Uwekezaji iliyo chini ya
Ofisi ya Waziri Mkuu kwa ajili ya kuifanya Tanzania kuwa ni mahali bora
na salama kwa wawekezaji na wafanyabiashara.
Waziri
Mkuu ameyasema hayo leo (Jumatano, Julai 3, 2019), wakati akizungumza
na Balozi wa Vietnam nchini, Balozi Doanh. Mazungumzo hayo yamefanyika
kwenye Ofisini kwa Waziri Mkuu, Magogoni jijini Dar Es salaam.
Waziri
Mkuu ametumia fursa hiyo kuwaalika wafanyabiashara na wawekezaji kutoka
nchini Vietnam waje kuwekeza katika sekta ya viwanda hususani vile
vinavyotumia malighafi za mazao ya kilimo yanayolimwa hapa nchini. Hatua
hiyo itawawezesha wakulima wa Tanzania kuwa na soko la uhakika la mazao
yao.
“Serikali
imeendelea kuondoa vikwazo vya kuanzisha na kuendesha biashara kwa
kupitia upya sheria, kanuni na taratibu za biashara na kuzifuta
zile ambazo zimethibitika kuwa zinayafanya mazingira ya biashara na
uwekezaji nchini kuwa magumu.”
Waziri
Mkuu amesema kwa kuwa nchi ya Vietnam imepiga hatua kubwa katika ujenzi
na uendeshaji wa viwanda vya nguo, Tanzania ingefurahi kuona kwamba
viwanda vya aina hiyo vinajengwa hapa nchini na wawekezaji kutoka nchi
hiyo.
Amesema
kuwa ununuzi wa mazao ya kilimo kama vile pamba, koroshao, kahawa na
tumbaku ni fursa nyingine ya kibiashara ambayo wafanyabiashara wa
Vietnam wanakaribishwa kuichangamkia hapa nchini.
Akizungumzia
kuhusu soko la korosho Waziri Mkuu amesema Tanzania ina korosho za
kutosha na inawakaribisha wafanyabiashara kutoka Vietnam waje kuzinunua.
Kwa wale wenye uwezo wa kujenga viwanda vya kuchakata korosho nao
amewakaribisha na kuahidi kuwa Serikali iko tayari wakati wote
kuwasaidia.
Kwa upande wake,
Balozi Doanh alitumia fursa hiyo kumweleza Waziri Mkuu juu wa ujio wa
Naibu Waziri Mkuu wa Vietnam, Mhe. Trinh Dinh Dung anayetarajiwa kufanya
ziara yake ya kikazi nchini kuanzia Julai 9 hadi 11 mwaka huu.
Alisema Naibu Waziri Mkuu huyo anatarajiwa kuambatana na wafanyabiashara wasiopungua 20 kutoka kampuni kubwa za nchini Vietnam.
Nchi
za Vietnam na Tanzania zilianzisha uhusiano wa kidiplomasia mwaka 1965.
Mwaka 1984, Vietnam ilifungua ofisi ya Ubalozi wake hapa nchini kwa
muda na kuufungua upya mwaka 2003.
No comments:
Post a Comment