HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 05, 2019

RT yaendesha mafunzo ya ukocha UDSM

Mkufunzi wa kozi ya riadha Dk. Hamad Ndee, akiendesha mafunzo ya rmchezo huo kwenye viwanja vya Chuo Kikuu Dar es Salaam leo.
Dar es Salaam, Tanzania
SHIRIKISHO la Riadha Tanzania (RT), kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), limeendesha Kozi ya Ukufunzi (IAAF Level 1 Lecturers).

Akizungumza na Waandishi wa Habari kwenye viwanja vya michezo UDSM, Mkufunzi wa kozi hiyo anayetambuliwa na IAAF Dk. Hamad Ndee, alisema kozi imeshirikisha washiriki 25 ambao ni wanafunzi wa mwaka wa pili wanaochukua shahada ya Phisical Education and Sports Sciences.

Dk. Ndee, alisema hivj karibuni IAAF iliamua kubadili mfumo wake wa ngazi za ualimu wa riadha kutoka nne hadi tatu kwa kuunganisha ngazi ya kwanza na ya pili.

"Ngazi hizi mpya ni 'Level 1 Coach U 16, Level II Coach U 20 na Level III Coach 20 Above'. Ili kuandaa walimu IAAF Level 1 Lecturers wa kufundisha ualimu wa riadha katika nchi mbalimbali IAAF ilianza kuendesha mafunzo hayo maalumu tangu mwaka 2016...Tayari nchi nyingi pamoja na Tanzania zimepata walimu hawa 'IAAF Level 1 Lecturers'," alisema Dk. Ndee.

Alisema moja ya majukumu ya Shirikisho la Riadha Tanzania ni kutayarisha ni kutayarisha Walimu wa Riadha katika ngazi zote.

"Hivyo basi mpango wa RT wa muda mrefu ni kuendesha mafunzo ya ngazi ya kwanza 'Level 1 Coach U 16' na hatimaye ngazi zote nchini kwa walimu wa riadha. 
RT itashirikiana na mikoa kwa kadri iwezekanavyo ili kuendesha mafunzo haya ya ualimu wa riadha kwa ngazi zote, lakini kwa kianzia tumeanza kwa kushirikiana na Idara ya Elimu kwa Michezo na Sayansi ya Michezo ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwa wanafunzi wanaotaka kuwa makocha wa mchezo wa riadha," alisema Dk. Ndee ambaye pia ni Makamu wa Pili wa Rais RT-Ufundi na Mkufunzi Mwandamizi UDSM.

Nao washiriki wa kozi hiyo ambayo ilifikia tamati jana, walisema wamepata ujuzi mkubwa katika mchezo wa riadha tofauti na walivyokuwa wakiuchukulia mchezo huo kwa kudhani riadha ni kukimbia tu.

Mmoja wa washiriki hao, Nyamizi Lucas, alisema atayatumia kivitendo mafunzo hayo kwa kuibua na kuviendeleza vipaji vya riadha nchini kwa manufaa ya vijana na Taifa kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment

Pages