HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 05, 2019

Wananchi watakiwa kufika banda la Costech kumuona mtengenezaji wa mitambo ya kuchuja maji taka yanayotoka viwandani

Muonekano wa banda la Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Biocon Afrika Ltd ambayo ushughulika na utengenezaji wa mitambo ya wa kuchuja maji taka ya viwandani, Profesa Karoli Njau akiwaelekea wananchi jinsi mtambo unavyofanya kazi.

 
Na Janeth Jovin

WANANCHI wametakiwa kufika katika banda la Tume ya Taifa ya  Sayansi na Teknolojia  (Costech)  kwa lengo la kumuona  Mkazi wa Arusha aliyetengeneza mitambo ambayo inachuja  maji taka yanayotoka  viwandani kisha kupata nishati ya bayogesi inayoweza kuzalisha umeme na gesi zinazotumiwa katika viwanda.

Akiwa katika maonesho ya 43 ya Biashara ya kimataifa DITF katika  banda hilo la COSTECH, mbunifu huyo ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Biocon Afrika Ltd ambayo ushughulika na utengenezaji wa mitambo hiyo, Profesa Karoli Njau  anasema tayari ameshatengeneza mtambo huo wa kuchuja maji taka katika machinjio yaliyopo Nyakato jijini Mwanza.

Anasema mtambo huo haufanyi kazi yakuchunja maji taka tu bali pia uwasaidia kupata nishati ya bayogesi ambayo inaweza kuzalisha umeme.

"Tumeshatengeneza mitambo miwili mikubwa mmoja ndo huo uliyopo Mwanza na mwingine upo katika Kiwanda cha kutengeneza divai Arusha, mtambo mwingine mkubwa ambao unakuja ni kwa ajili ya kiwanda cha Kahawa cha Nairobi Kenya, " anasema.

Hata hivyo anasema gharama za mitambo huo unategemea na wingi wa maji taka na uchafu uliyopo kwenye maji hao.

"Gharama zetu zinategemea wingi wa maji taka na uchafu uliyopo kwenye maji ila gharama za mitambo hii kwa midogo ni kati ya Milioni 100 hadi 150.," anasema.

No comments:

Post a Comment

Pages