HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 06, 2019

Suma JKT yaleta dawa ya wezi wa magari

Ofisa Masoko wa Kampuni ya Suma JKT Guard, Evance Kilepo, akizungumza na mmoja wa watu waliotembelea banda lao katika Maonyesho ya Sabasaba.


Na Janeth Jovin

KUTOKANA na uwepo wa changamoto ya watu kuibiwa magari,  Kampuni ya ulinzi ya SumaJKT Guard imeleta kifaa maalum chenye uwezo wa kuzima, kuwasha na kukata mfumo wa mafuta katika gari kwa kutumia simu ya mkononi.

Kifaa hicho ambacho ufungwa katika gari la mtu kinaelezwa kuwa ndio mkombozi kwa watanzania katika kuhakikisha ulinzi wa mali zao hasa  wale wote wanaokumbana na wezi wanaowabia magari. 

Akizungumza katika maonesho ya 43 ya kimataifa ya biashara Sabasaba,  Meneja Masoko wa kampuni hiyo Kapten Ashery Mollel anasema kifaa hicho pia kinauwezo wa kurekodi na kuongea na mtu aliyekuwepo ndani ya gari.

Anasema kifaa hicho kinamfumo wa GPS ambao umeboreshwa ambapo kinafungwa kwenye gari kisha chipu yake ambayo ndio umuwezesha mtu kuzima, kuwasha au kukata mfumo wa mafuta kuwekwa katika simu janja (smartphone) ya mtu ya mkononi.

Anasema kifaa hicho wamekinunua kutoka nje na kampuni yao hiyo inauwezo wa kukifunga katika gari kwa utaalamu zaidi.

"Kifaa hichi tumekileta hapa sabasaba kwa sababu tunaamini ndipo mahali watu wengi wanakuja hivyo watapata fusra ya kujifunza na kuona jinsi kinavyofanya kazi,  kifaa hiki mtu akitaka tunamfungia na tunahakikisha tunakiweka sehemu ambayo mwenye gari pekee ndio anaweza kukiona, " anasema

Aidha anasema gharama ya kifaa hicho kimoja ni Sh. 350,000 na gharama ya kukifunga katika kila gari moja ni Sh. 150,000.

No comments:

Post a Comment

Pages