HABARI MSETO (HEADER)


Breaking

July 01, 2019

TADB yawahakikishia wakulima wa kahawa

 Mkuu wa Mkoa wa  Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gagiuti (kulia), akiangalia jinsi kahawa invyopimwa mara ya kuzindua msimu wa ukusanyaji  kahawa huko Nkwenda Kyerwa hivi karibuni. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB),
Bw. Japhet Justine ambaye amewahakikishia wakulima malipo yao yatafanywa kwa wakati.
Mkuu wa Mkoa wa  Kagera, Brigedia Jenerali Marco Gagiuti (kushoto), akimsikilia mkulima wa kahawa  jinsi kahawa inavyopimwa mara ya kuzindua msimu wa ukusanyaji  kahawa huko Nkwenda Kyerwa hivi karibuni. Nyuma yake aliyevaa T-shirt ya kijani ni Mkurugenzi Mtendaji wa  Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Japhet Justine ambaye amewahakikishia wakulima malipo yao yatafanywa kwa wakati.


Na Mwandishi Wetu, Kagera

MSIMU wa ukusanyaji wa kahawa  kwa mwaka 2019/2020 kutoka  kwa wakulima hadi Vyama vya Msingi umezinduliwa  rasmi  Mkoani Kagera huku Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania(TADB) ikiwahakikishia wakulima wa zao hilo kupata malipo yao kwa wakati. Katika msimu uliopita Benki ya Maendeleo ya Kilimo ilitoa zaidi ya shilingi bilioni 30 ambazo ziliwanufaisha  moja kwa moja wakulima
148,000. 
 
Akizungumza mara baada ya kuzinduliwa msimu wa ukusanyaji wa kahawa ambapo Vyama Vikuu vya Ushirika  vya KCU 1990 Limited na KDCU Limited kutangaza malipo ya awali kuwa shilingi 1,100 kwa kilo moja ya
maganda,Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Japhet Justine amesema benki yake itatoa fedha kwa wakati na kumfikia mkulima moja kwa moja kupitia
mfumo wa benki. 
 
“Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa alizindua akaunti jumuishi za wakulima ili wakulima wasikatwe fedha zao hata kama ni senti moja ilipwe moja kwa moja kwa mkulima na sisi kama TADB tutahakikisha tunalipa fedha hizo kupitia akaunti za benki,” alisisitiza Bw. Justine. 
 
Bw. Justine aliwathibitishia wakulima kuwa TADB imejipanga kimkakati kuhakikisha kuwa wakulima wananufaika na kuwepo kwa benki ikiwemo kupata malipo yao kwa wakati na kumudu kununua pembejeo za kilimo. “Kama benki ya maendeleo ya kilimo hapa nchini, tumejipanga kuchagiza mageuzi katika sekta ya kilimo ili kufanikisha azma  ya Serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi wa Rais Dkt. John Pombe Magufuli ya kujenga uchumi wa kati na viwanda ifikapo mwaka 2025,” alisema.

Akizindua rasmi msimu huo wa ukusanyaji wa kahawa hivi karibuni Mkuu wa Mkoa wa Kagera Brigedia Jenerali Marco E. Gagiuti wilayani Kyerwa Nkwenda, aliwahakikishia wakulima serikali imejipanga kuondoa changamoto zote zilizojitokeza msimu uliopita na mkulima atanufaika na kahawa yake na kulipwa kwa wakati.

Akizungumza na wakulima wa kahawa na wananchi waliokusanyika kumsikiliza Nkwenda Kyerwa alisema kuwa tayari Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera tayari vimepewa Shilingi bilioni saba na TADB aidha, wakulima
ambao tayari wamekusanya kahawa yao kwenye Vyama vya Msingi wataaanza kulipwa malipo ya awali ya shilingi 1,100/-kwa kila kilo kuanzia Julai 1, 2019.

“Msimu tutahakikisha kuwa wakulima wanalipwa fedha zao kwa wakati ikiwa ni pamoja na kuhakikisha fedha hizo hazipiti katika mikono mingi ya viongozi wa Vyama vya Msingi,” alisema na  kuongeza kuwa mkulima
atalipwa fedha zake moja kwa moja kupitia akaunti yake.

Katika kuondoa changamoto za msimu uliopita wa mwaka 2018, Brigedia Gaguti alikikagua Chama cha Msingi Rwabwere na kujionea namna ya kupima kahawa za wakulima na kuagiza kuwa lazima kilo zote na pointi
ziandikwe na mkulima ilikupunguza malalamiko.

Kuhusu fedha za mazidio za wakulima, Mkuu wa Mkoa huyo alisema fedha hizo zisitolewe maamuzi na viongozi wa vyama vya msingi bali wakulima wenyewe ndiyo waamue zitumike zifanyi nini. 
 
Aidha, Brigedia Gaguti na ujumbe wake walikagua pia shamba bora la mkulima Bw. Abdu Ndegeza na kuona kahawa bora na zilizokomaa zikivunwa. 
 
Tayari Chama Kikuu cha Ushirika cha KDCU Limited tayari kimekusanya kilo milioni 3,200,000 matarajio yake ni kukusanya kilo milioni 35,000,000. Msimu wa Mwaka jana 2018 Vyama Vikuu vya Ushirika Mkoani Kagera vilikusanya jumla  kilo milioni 58.9  na msimu huu vyama hivo vinatarajia kukusanya zaidi kilo milioni 52.

No comments:

Post a Comment

Pages